Posts

Showing posts from July, 2015

Basata wamfungia shilole kufanya kazi yoyote ya kisanaa mwaka mzima

Image
Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) limemfungia Shilole kutojihusisha na kazi yoyote ya sanaa kwa muda wa mwaka mmoja. Barua kutoka BASATA inasema hivi "Tarehe 9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili‘ ‘BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa maelezo yako‘ ‘Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho lako huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja...

SZCZESNY AKOPESHWA AS ROMA, YOUNG KUTUA SPURS?

Image
WAKATI Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny amejiunga na moja ya Vigogo wa Italy, Klabu ya AS Roma , kwa Mkopo wa Msimu mmoja, zipo habari zilizozagaa huko London kuwa Tottenham Hotspur inamtaka Winga wa Manchester United, Ashley Young. SZCZESNY AKOPESHWA AS ROMA Msimu uliopita, Szczesny, mwenye Miaka 25, alipoteza namba kwa David Ospina na Msimu huu Arsenal imejiimarisha kwenye safu ya Kipa kwa kumnunua Mwezi uliopita Kipa kutoka Chelsea Petr Cech. Szczesny, Kipa wa Kimataifa wa Poland ambae ameidakia Arsenal mara 180, ameanzia Timu za Vijana za Timu hiyo mara baada ya kujiunga Mwaka 2006 akitokea Klabu ya Nchi kwao Legia Warsaw. Licha ya kumtoa kwa Mkopo, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amedai Kipa huyo bado anaweza kuwa hazina kwao kwa vile atapata uzoefu zaidi huko Italy. YOUNG KUTUA SPURS? Winga wa Manchester United Ashley Young anavumishwa kutakiwa kwa udi na uvumba na Klabu ya London Tottenham Hotspur. Ingawa habari hizi hazijathibitishwa, Spurs wamesemwa kuwa wa...

maneno ya lowasa kwenye hotuba yake alipokuwa akikaribiswa rasmi chadema

Image
[ pichani akionekana mwenyekiti wa chadema taifa mhe. freeman mbowe akisalimiana na aliyekuwa waziri mkuu mstaafu na mbunge wa monduli mhe. edward lowasa mara baada ya kutangazwa rasmi kama mwanachama wa chadema hapo jana] Ndugu waandishi wa habari na ndugu Watanzania wenzangu. Yamepita majuma mawili tangu mchakato wa kuchagua mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ukamilike. Nimetumia muda huu kutafakari kwa kina yaliyotokea Dodoma na hatima yangu katika siasa nchini. Ninajua marafiki wengi na wananchi wenzangu wanaoniunga mkono wamekuwa wakisubiri kwa hamu nitoe kauli. Nilipokuwa natangaza nia ya kugombea urais kule Arusha, nilieleza nia yangu ya kuanza mchakamchaka wa maendeleo ya nchi yetu na kuondokana na umaskini. Pamoja na yaliyotokea Dodoma, azma hii bado iko palepale. Lakini nianze kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema aliyetupa sisi pumzi ya kuendelea kuwa wazima wa afya njema hadi hivi sasa. Nawashukuru pia mke ...

Drogba kucheza na Lampad ligi moja marekani

Image
I Didier Drogba mwishowe akamilisha uhamisho wake kwa Impact de Montreal Impact de Montreal siku ya Jumatatu ilitangaza kuwa imekamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba. Staa wa Ivory Coast alikuwa bila klabu baada ya kuondoka Chelsea mwezi Mei, lakini sasa ataungana na mchezaji mwenzake wa zamani Frank Lampard katika Ligi ya Marekani. "Ni heshima kumkaribisha Didier Drogba kwa Impact," Rais wa Montreal Joey Saputo aliiambia tovuti rasmi ya klabu. "Kutokana na mazungumzo ya awali tuliyofanya naye, nilihisi kwamba kwa kweli alikuwa anataka kucheza katika Montreal. Hii ni moja ya siku kubwa katika historia ya klabu na itakuwa ya manufaa katika nyanja zote." Drogba alicheza mechi 381, na kushinda mataji manne ya Ligi Kuu ya Uingereza katika awamu mbili akiwa na klabu hiyo ya London.

Mourinho asema hazard ni bora kuliko CR7

Image
Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho yaamini kwamba Eden Hazard alikuwa na msimu bora mwaka jana kuliko staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Kiungo wa Ubelgiji alitoa mchango muhimu kwa Chelsea kushinda Ligi Kuu ya Uingereza na Capital One Cup msimu uliopita na alipata kutajwa na PFA kuwa mchezaji bora wa mwaka baada ya kufunga mabao 19 katika kampeni. Wakati huo huo, Ronaldo alifunga mabao 62 lakini Real Madrid imeshindwa kushinda taji lolote la ndani katika Hispania au Ligi ya Mabingwa, na ndiyo maana Mourinho anamweka Hazard katika kiwango cha juu msimu upitao. "Msimu uliopita, ndiyo. Licha ya kuwa Ronaldo alikuwa mzuri. Alikuwa staajabu. Yeye alifunga idadi ya ajabu ya mabao,'' Mourinho alisema. "Mimi sisemi kuwa si mzuri. Nasema tu kwamba, kwa maoni yangu binafsi, kila mchezaji wa mpira duniani anapaswa kuelewa kuwa timu inakuwa mbele na hakuna mataji. Eden anakuja na hadhi kubwa sasa na alichaguliwa katika wachezaji 10 bora katika Ulaya mwaka jana. Kwa...

VAN GAAL KUONDOKA KWA SABABU YA MKE

Image
Meneja wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa huenda akaondoka katika kilabu ya Manchester United mwisho wa kandarasi yake ya miaka mitatu ili kutimiza ahadi aliyotoa kwa mkewe. Alipoulizwa iwapo ataongeza kandarasi yake kwenye klabu hiyo yenye maskani yake Old Traford ,raia huyo wa Uholanzi ameiambia BBC kwamba ataondoka mwisho wa kandarasi yake mwaka 2017. ''Nilimuahidi mkewe wangu.hatuna miaka mingi iliosalia,na hiyo ndio sababu'', alisema meneja huyo mwenye umri wa miaka 63. ''Nimefanya kila kitu katika maisha yangu kama mkufunzi''. Alipulizwa iwapo kuna uwezekano wa yeye kusalia katika klabu hiyo,alijibu kwamba hawezi kutoa jibu lolote kwa kuwa mkewe amekasirika sana. ''Nakiri kwamba nilimwambia kuwa ningestaafu ifikiapo miaka 55 lakini mapaka sasa nikiwa na umri wa miaka 63 bado naendelea na ukufunzi na wiki ijayo natarajia kufikisha miaka 64''alisema meneja huyo.

headline kubwa za magazeti ya leo

Image

Mtoto wa Whitney Houston ‘Bobbi Kristina’ afariki

Mtoto wa Marehemu Whitney Houston na Bobby Brown ‘Bobbi Kristina’ amefariki dunia akiwa na miaka 22. Bobbi amefia nje ya mji wa Atlanta kwenye nyumba ya uangalizi wa wagonjwa alipokuwa akiishi toka June 24 baada ya familia yao kuacha matibabu yote kutokana na ushauri wa daktari kuwa Bobbi hataweza kupona. Kwa majonzi makubwa taarifa hii imethibitishwa na familia ya Bobbi Kristina na mazishi yameanza kupanga. Kwa upande mwingine polisi wameanza uchunguzi juu ya anayedai ni mume wa Bobbi ‘Nick Gordon’ akiwa miongoni mwa watu wanaohisiwa kutengeneza mazingira ya kumua Bobbi. Bobby Brown amesema  “ Sasa hivi tunachotaka ni kumzika binti yetu ili ampumzike kwa amani lakini upelelezi wa kifo chake utaanza rasmi baada ya mazishi haya, Mtu yeyote aliyehusika kusababishia kifo cha mwanangu lazima sheria ichukue mkondo wake”.

Diamond Platnumz ashinda tuzo nyingine Afrika Kusini ‘African Achievers Awards’.

Image
Msani wa bongo fleva Diamond Platnumz ameshinda tuzo ya ‘African Achievers Awards’ katika tuzo zilisofanyika Afrika kusini, Tuzo aliyoshinda Diamond ni ya Artist of the Year ‘Msanii Bora Wa Mwaka’.

Dimaria huyoooo PSG

Image
Di Maria amewaambia Man United anataka kujiunga na PSG Stoo ya United ikiwa na maski za Robin van Persie, Di Maria na Radamel Falcao ambazo ndizo pekee zinazouzwa kwa bei rahisi kabisa. Angel di Maria amewaambia Manchester United kwamba anataka kuhamia kunako klabu ya Paris Saint-Germain -huku Laurent Blanc akisisitiza kuwa na nia ya kunasa Muargentia huyo hata ikibidi wiki hii.  Mabingwa hao wa Ufaransa, awali walitoa ofa ya pauni milioni 46.5 na inasemekana kuwa mpaka kufikia siku ya Jumatatu dili hilo litakuwa limekamilika. Kocha wa Manchester United aliwaambia wachezaji wake mapema kabisa kabla ya mchezo dhidi ya Barcelona kwamba Di Maria yuko mbioni kujiunga na PSG baada ya kukacha kujiunga na wenzake kwa ajili ya mchezo huo huko Santa Clara.  Marcos Rojo kwa upande wake hakuwepo pia lakini yeye taarifa zake ziko wazi kwamba ana matatizo katika pasi yake ya kusafiria lakini hata hivyo anaweza kukumbana na hatua za kinidhamu kutoka kwa koch...

Louis van Gaal alimaliza kumsajili mshambuliaji kwa siri

Image
Memphis Depay yadhaniwa kuwa mshambuliaji wa Manchester United aliyesainiwa na Louis Van Gaal kisiri katika kiangazi hiki, ripoti kutoka Uholanzi zinasema. Anapozungumza katika mkutano wa watangazaji habari nchini Marekani wiki iliyopita, Louis Van Gaal aligusia kuhusu mshambuliaji staajabu wake aliyesajili kiangazi hiki. Lakini baada ya ushindi wa United wa mabao 3-1 dhidi ya San Jose Earthquakes,Van Gaal alisema kuwa maneno yake yalielezwa vibaya, huku akisema kuwa hakusema kuwa alinunua mshambulizi mpya. “Sijui kama nahitaji kununua mshambuliaji. Nimesoma katika vyombo vya habari kwamba ni mshambuliaji fumanio,” alisema. “Hapana, hivyo sikuvisema. mnasema hivyo, kwa sababu jibu langu ni kama lile. Hapana, namaanisha kitu kingine.” Kwa mujibu wa gazeti la Uholanzi Metro, Louis Van Gaal atamtumia Memphis Depay kama mshambuliaji msimu ujao. Memphis Depay alifunga bao lake la kwanza kwa Manchester United katika ushindi wa 3-1 dhidi ya San Jose Earthquakes katika maandalizi ya ms...

chadema fomu za urais za moto

Image
Wakati leo saa 10 jioni ndiyo muda wa mwisho uliopangwa kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais ndani ya Chadema, hadi sasa hakuna mwanachama hata mmoja aliyejitokeza kuzichukua. Badala yake zimetolewa kauli tofauti kuhusu kusuasua kwa mchakato wa kumpata mgombea urais hadi chama hicho kulazimika kusogeza mbele tarehe ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu. Hali hiyo inazidisha sintofahamu iliyougubika mchakato wa urais ndani ya chama hicho na ndani ya Ukawa, kuwa huenda kuna ‘mtu wa nne’ anayesubiriwa kutoka nje ya chama hicho, kama ilivyoripotiwa na gazeti hili, wiki iliyopita. Likikariri chanzo cha kuaminika ndani ya Ukawa, gazeti liliandika kuwa huenda umoja huo na hasa Chadema, wanasubiri mgombea kutoka nje ya chama kwa kuwa hata baada ya wajumbe wa vikao vya mashauriano kukubaliana kuwa mgombea wa Ukawa awe Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, baadhi ya wajumbe kutoka katika chama hicho wanadaiwa kukataa kutangazwa kwake. Hata baadaye wa...

» D’Banj diamond ananizungusha collabo

Image
Muimbaji mkubwa wa Nigeria, D’Banj amemlalamikia Diamond kwa kumzungusha kufanya naye collabo. Kokomaster amesema kuwa toka walipokutana na Diamond walizungumza na kukubaliana kufanya collabo lakini amekuwa akimpiga chenga mpaka sasa.    Star huyo ambaye aliibuka na tuzo ya ‘MAMA Evolution’ katika MTV MAMA 2015, ameongeza kuwa kabla mwaka huu haujaisha anaamini collabo hiyo itakuwa tayari imefanyika. Diamond ametoa sababu za kuchelewa kufanya collabo na D’Banj.   “Tulikutana kule kwenye Do Agric tukafanya Cocoa na Chocolate, tukatakiwa kufanya nyimbo ya mimi na yeye lakini nikaogopa ukianza na msanii mkubwa sana itakuwa kurudi tena itakuwa tabu lazima uanze kwa ngazi kwa ngazi kwa ngazi ili kesho na kesho kutwa ukitoa nyimbo uonekane unazidi kupanda, sio unafanya nyimbo na mkubwa halafu kesho unashuka, nafikiri ndio ikawa sababu pia nyimbo yangu ya kwanza sikuweza kufanya na yeye ya kwanza.

Arsene Wenger anafikiria kuhusu kustaafu? Huwa inamjia akilini, alafu…

Image
Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger amedumu na klabu ya Arsenal kwa zaidi ya miaka kumi na tano toka alipojiunga nayo 1996, Wenger anakuwa kocha wa pili katika historia ya Ligi Kuu Uingereza kudumu na timu kwa muda mrefu baada ya kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ambaye amestaafu mwaka 2013. Kufuatia kustaafu kwa Sir Alex Ferguson mwaka 2013 kumekuwa na maswali mengi kuhusiana na Wenger lini atastaafu, wengi wanaamini Wenger alikuwa na uwezo wa kuifundisha Arsenal kutokana na rekodi alioweka ndani ya miaka tisa ya mwanzo klabuni hapo, Wenger alishinda mataji 7 lakini miaka kumi baadae Wenger ameishia kutwaa mataji mawili pekee rekodi inayotia mashaka na uwezo wake. Wengi walitazamia kuwa kuna uwezekekano wa Wenger kustaafu kwa miaka ya hivi karibuni lakini alichojibu kuhusu suala la yeye kustaafu bado linawaacha watu njia panda ya lini atastaafu. “Kustaafu? ndio wakati mwingine huwa inanijia akilini lakini sio zaidi ya sek...

HATMA YA BALOTELLI IPO HIVI KAMA ALIVYOSEMA BRENDAN RODGERS

Image
Liverpool inasajili sana wachezaji hasa ambao wanaocheza namba moja na Balotelli. Pia hivi karibuni Balotelli alimtetea Raheem baada ya kuhama Liverpool kwenda Manchester city na mashabiki wa Liver walimshambulia Balotelli kwenye mitandao. Lakini Balotelli ameachwa kwenye pre season kwasababu ya kufiwa na baba yake mlezi lakini hivi sasa yupo kwenye mazoezi kwenye uwanja wa Melwood. Rogers alipoulizwa kuhusu hatma ya mchezaji huyo alisema, “Mario hayupo kwenye tour yetu lakini anafanya mazoezi kwa bidii na baadhi ya wachezaji uwanjani. Sijui future yake iko vipi lakini ninavyojua future yake ipo mikononi mwake kwa kufanya mazoezi kwa bidii. Lakini najua anafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kujiandaa kwa msimu ujao” Namba ya Balotelli ipo kwenye ushindani mkubwa baada ya usajili ambao Liverpool wameufanya na ambao wanatarajia kuufanya kwa kutoa ofa ya £32.5 million kumsajili Christian Benteke   source shaffih dauda

wafahamu hapa wanaotaka kuwania ubunge wilaya ya mbeya mjini kupitia ccm

Image
source mbeya yetu

AJALI Mbaya ya Basi Mkoani Dodoma, Abiria zaidi ya 20 Wamefariki Dunia na 38 Wamejeruhiwa...

Image
Taarifa kutoka mkoani Dodoma zinasema zaidi. Abiria zaidi ya 20 wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo huku zaidi ya abiria 38 wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya SIMIYU EXPRESS walilokua wakisafiria kutoka Mwanza kwenda DSM kupasuka tairi na kuacha njia na kugonga mbuyu na kisha kupinduka. Taarifa zinasema ajali hiyo ni mbaya sana kuwahi kutokea mkoani Dodoma, hadi hivi sasa bado kuna miili haijatolewa kwenye mabaki ya basi hilo kutokana na kuharibika vibaya na kubaki mithili ya nyama. MWENYEZI MUNGU AZILAZE MAHALA PEMA PEPONI ROHO ZA MAREHEMU NA KUWAPA NGUVU FAMILIA ZOTE ZA MAREHEMU AMEEN

Mziki wa Yanga utakaokwaana na Telecom kombe la Kagame huu hapa

Image
KOMBE LA KAGAME || KUNDI A || 2015. YANGA SC (Tanzania) vs TELECOM (Djibout) KIKOSI CHA KWANZA YANGA. 1.Ally Mustafa Mtinge "Barthez" 2. Mbuyu Twite. 3. Hadji Mwinyi Ngwali. 4.Kelvin Patrick Yondani 5.Nadir Haroub Ally "cannavaro" 6.Salum Abo Telela "Master" 7.Simon Happygod Msuva 8.Haruna Niyonzima "Fabregas" 9.Jocelyn Amiss Tambwe. 10.Deus David kaseke. 11.Geofrey mwashiuya "Lunyamila Jr" SUB. Deo Munishi "Dida" Juma Abdul Pato Ngonyani. Joseph Tetteh Zuttah Oscar Fanuel Joshua Kpah Sean Sherman Andrey Coutinho

Picha,The Game kapania, anarekodi album ata akiwa uwani.

Image
Rapa The Game ameonyesha juhudi na ubunifu wa kutopoteza muda wakatiwakurekodi album yake mpya ya The Documentary 2. The Game ameweka picha akiwa uwani ila bado anarekodi nyimbo kama kawaida, kitu ambacho kimechukuliwa kama kituko na baadhi ya mashabiki wake. Album ya “The Documentary 2″ inafanywa na producers Dr. Dre, Timbaland, Pharrell, na Swizz Beatz.

WAYNE ROONEY KURUDI KUICHEZEA EVERTON!

Image
STRAIKA wa Manchester United Wayne Rooney amekubali kuichezea Everton kwenye Mechi maalum ya kumuenzi Mchezaji wa zamani wa Klabu hiyo Duncan Ferguson. Rooney, mwenye Miaka 29, ataichezea Everton Mechi hiyo hapo Agosti 2 dhidi ya Villarreal huko Goodison Park Jijini Liverpoool. Baada ya kuihama Everton Mwaka 2004 na kwenda Man United, Rooney, alieanzia Soka lake la utotoni kwenye Chuo cha Everton, amekuwa hakaribishwi vyema Goodison Park na Mashabiki wa Timu hiyo na Mwaka 2008 aliamsha hasira kubwa aliporudi Goodison Park kucheza dhidi ya Everton na kuonekana akibusu Beji ya Man United. Akikaririwa kwenye Tovuti ya Everton, Rooney amesema: "Nilipokuwa nikikua huko Croxteth, Duncan Ferguson alikuwa shujaa wangu. " Rooney ameongeza: "Njia bora ya kumshukuru Duncs kwa yote aliyonifanyia mimi ni kuja kucheza hii Mechi ya kumuenzi. Hata kama asingeniita kuja kucheza ningekuja kumshukuru!" Duncan Ferguson ni mmoja wa Malejendari wa Everton aliyoichezea kwa vi...

AFRIMMA:Diamond atajwa kwenye vipengele 7 wamo pia Ally Kiba,Ommy Dimpoz,Vannesa Mdee na Mrisho Mpoto.

Image
Majina ya watakaoshindana katika tuzo za AFRIMMA yametangazwa leo…kwa Tanzania nzima tunawakilishwa na Diamond Platnumz,Vanessa Mdee, Ommy Dimpoz na Mrisho Mpoto. Diamond yupo katika Categories saba…Cheki majina yote hapa Chini… 1. Best Male West Africa Davido (Nigeria) Serge Beynaud (Ivory Coast) Wizkid (Nigeria) Sarkodie (Ghana) Flavour (Nigeria) Carlou D – (Senegal) Olamide (Nigeria) Stonebwoy (Ghana) 2. Best Female West Africa Yemi Alade (Nigeria) Wiyaala (Ghana) Tiwa Savage (Nigeria) Viviane Chidid (Senegal) Teeyah (Ivory Coast) Becca (Ghana) Almok (Togo) Efya (Ghana) 3. Best Male East Africa Eddy Kenzo (Uganda) Jaguar (Kenya) Diamond Platnumz (Tanzania) Bebe Cool (Uganda) Jackie Gosse (Ethiopia) Ali Kiba (Tanzania) Dynamq (Sudan) 4. Best Female East Africa Khadija Kopa (Tanzania) Aster Aweke (Ethiopia) Victoria Kimani (Kenya) Vanessa Mdee ( Tanzania) Juliana Kanyamozi (Uganda) STL (Kenya) Irene Ntale (Uganda) ...