AJALI Mbaya ya Basi Mkoani Dodoma, Abiria zaidi ya 20 Wamefariki Dunia na 38 Wamejeruhiwa...

Taarifa kutoka mkoani Dodoma zinasema zaidi.
Abiria zaidi ya 20 wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo
huku zaidi ya abiria 38 wakijeruhiwa vibaya
baada ya basi la kampuni ya SIMIYU EXPRESS
walilokua wakisafiria kutoka Mwanza kwenda
DSM kupasuka tairi na kuacha njia na kugonga
mbuyu na kisha kupinduka.
Taarifa zinasema ajali hiyo ni mbaya sana
kuwahi kutokea mkoani Dodoma, hadi hivi sasa
bado kuna miili haijatolewa kwenye mabaki ya
basi hilo kutokana na kuharibika vibaya na
kubaki mithili ya nyama.
MWENYEZI MUNGU AZILAZE MAHALA PEMA
PEPONI ROHO ZA MAREHEMU NA KUWAPA
NGUVU FAMILIA ZOTE ZA MAREHEMU AMEEN

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP