RONALDO AMZUNGUMZIA MAMA WA MWANAE PAMOJA NA KURUDI MAN UNITED
Ronaldo amesema hatomtaja mama wa mtoto wake mpaka atakapoona muda umefika Mchezaji Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, amesema kamwe hatomtaja mama mzazi wa mtoto wake Ronaldo Jr. na kwamba muda ukifika atamuweka wazi huku mwanae pia akitakiwa kusubiri muda muafaka apate kumjua mama yake. Amesema kuwa amekua akishiriki mapenzi na warembo tofauti tofauti huku akikiri kuwa hiyo sio yeye tu bali ni tatizo kwa nyota wengi duniani kupitia maisha hayo huku akijinasibu kuwa kwasababu yeye ni mrefu, mwenye mwili mzuri wa mazoezi basi huwamaliza akina dada. Ronaldo ameweka wazi maisha yake binafsi wakati akifanyiwa mahojiano na Jonathan Ross Kuhusu Balon d’Or msimu huu, Ronaldo anasema Messi atatwaa tuzo hiyo kutokana na klabu yake ya Barcelona kutwaa makombe yote matatu iliyoshiriki msimu uliopita. Huku Ronaldo akisema ulikua ni msimu mzuri zaidi kwake binafsi kutokana na kufunga magoli mengi katika kila mashindano. Ronaldo ambaye alikua jijini London kwa utambulisho wa filam...