Posts
Showing posts from January, 2016
Unajua Messi kapiga chini Ofa ngapi za Real Madrid? Jibu hili hapa
- Get link
- X
- Other Apps
Mara ya mwisho kwa Real Madrid kumsajili mchezaji kutoka kwa mahasimu wao Real Madrid ilikuwa mnamo mwaka 2000 – wakati Luis Figo alipojiunga na Madrid kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi wakati huo – uhamisho ulikuza uhasama baina ya vilabu hivyo na tangu wakati huo hakujawahi kutokea biashara baina yao. Sasa takribani muongo mmoja upite tangu walipomchukua Figo Camp Nou – Real Madrid wamekuwa wakijaribu kwa nguvu zote kumsajili staa wa FC Barcelona, Lionel Messi, imeripotiwa. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Spain likiwemo gazeti la Cope – vimeripoti kwamba mshindi wa mara tano wa tuzo ya Ballon D’Or Lionel Messi, 28, amekuwa akipata maombi ya Madrid kujiunga nao lakini amekuwa akizipiga chini ofa za Los Blancos. Ripoti zinasema kwamba ofa ya kwanza ilitumwa mwaka 2011 wakati Real walipokuwa na hofu kwamba staa wao Cristiano Ronaldo alikuwa njiani kuelekea Man City. Real wakarudi tena mara ya pili wakati kiongozi wa juu wa klabu hiyo ambaye jina lake halikut...
RASMI: YANGA YAMREJESHA NIYONZIMA KUNDINI KUJIUNGA NA KIKOSI
- Get link
- X
- Other Apps
Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima (kulia) akizungumza na waandishi wa habari makaomakuu ya klabu hiyo, kushoto ni afisa habari wa Yanga Jerry Muro Kiungo wa kutumainiwa wa Yanga na timu ya taifa ya Rwanda amerejea kwenye timu yake ya Yanga baada ya kutimuliwa na uongozi huo kutokana na sababu za kinidhamu. Leo January 17, 2016 Niyonzima ameomba radhi kwa wanachama, viongozi na wachezaji wenzake kwa kile ambacho kilitokea miezi michache iliyopita. Niyonzima ameshaomba radhi mbele ya waandishi wa habari na kwa sasa anasubiri taarifa rasmi kutoka kwa uongozi wa Yanga kuhusu suala kusamehewa kwake. “Nitumie fursa hii kuwaomba radhi viongozi, wanachama, wachezaji wenzangu pamoja na mashabiki wa Yanga kutokana na yale yote yaliyopita nyuma. Mimi niliondoka kwenda kuichezea timu yangu ya taifa ya Rwanda lakini nilichelewa kurejea kwenye klabu yangu na hapo ndipo matatizo yalianza”, amesema Niyonzima. “Kiukweli nilikosea kwasababu sikutoa taarifa kwa timu yangu na ikachukua uamuzi wa...
Jinsi samatta alivyopokelewa uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere
- Get link
- X
- Other Apps
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza barani Afrika aliwasili jijini Dar usiku wa kuamkia leo majira ya saa na nusu. Licha ya kuwasili usiku kulikuwa na umati wa mashabiki pamoja na wazazi wake, viongozi wa TFF, wizara ya michezo, waandishi, mbunge Zuberi Zitto na wadau wengi waliofika mapema uwanja wa ndege tayari kwa kumpokea Samatta. Samatta akiwa na katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine mara baada ya kuwasili. Samatta, akiwa na babake, mamake na dadake (kushoto) Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo, Juliana Yasoda akimlaki Samatta
Askofu Pengo aitolea uvivu serikali kutibiwa nje
- Get link
- X
- Other Apps
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es salaam,Muadhama, Kardinali Pengo amesema kwamba ameridhishwa na huduma za afya zinazotolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), hivyo itakuwa ni vigumu kwa Serikali kumshawishi kwenda kutibiwa nje ya nchi. Kauli hiyo ilitolewa jana na Askofu Pengo ambaye amelezwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya MNH jijini Dar es Salaam kuanzia Januari Mosi, mwaka 2016 hadi sasa mara baada ya kuzungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambaye alimtembelea jana mchana ili kuweza kufahamu maendeleo ya afya yake. “Ninapenda kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania na kuwaondoa hofu kuwa hali ya Baba Askofu Pengo imeimarika na anaendelea vizuri, hajawekewa oxygen wala hajalazwa katika wodi ya uangalizi maalum(ICU) na ameridhika na huduma zinazotolewa,. “Ameridhika na huduma...
Idadi ya kura alizo pata samatta
- Get link
- X
- Other Apps
Mbwana Samatta ndio jina liliotajwa zaidi kwenye vinywa vya watanzania wengi na Afrika kiujumla ndani ya masaa kadhaa yaliyopita – baada ya mwanasoka huyo wa Kitanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika Anayecheza Ligi za Ndani ya Afrika. Ushindi wa Samatta, ambaye ni mshindi wa na mfungaji bora wa ligi ya mabingwa wa Afrika umetokana na kuwashinda wapinzani wake Zein Edin Farahat, Roger Assale, Robert Kidiaba, Moudather el Tahir,Mohammed Meftah, Kermit Erasmus, Felipe Ovono, Baghdad Bournedjah, na Abdeladim Khadrouf. Utaratibu wa CAF – Shirikisho la soka katika upigaji kura wa kumchagua mshindi wa tuzo hii unatokana na kura zilizopigwa na makocha wa timu za taifa au wakurugenzi wa ufundi wa vyama vya soka vya nchi za kiafrika. Kwa mwaka huu wachezaji wote hao waliotajwa hapo juu walipigiwa kura na matokeo ni kama yanavyoonekana kwenye mpangilio hapo chini. Mbwana Samatta alipata jumla ya kura 127 na hivyo kuongoza, a...