SZCZESNY AKOPESHWA AS ROMA, YOUNG KUTUA SPURS?

WAKATI Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny amejiunga na moja ya Vigogo wa Italy, Klabu ya AS Roma , kwa Mkopo wa Msimu mmoja, zipo habari zilizozagaa huko London kuwa Tottenham Hotspur inamtaka Winga wa Manchester United, Ashley Young.
SZCZESNY AKOPESHWA AS ROMA
Msimu uliopita, Szczesny, mwenye Miaka 25, alipoteza namba kwa David Ospina na Msimu huu Arsenal imejiimarisha kwenye safu ya Kipa kwa kumnunua Mwezi uliopita Kipa kutoka Chelsea Petr Cech.
Szczesny, Kipa wa Kimataifa wa Poland ambae ameidakia Arsenal mara 180, ameanzia Timu za Vijana za Timu hiyo mara baada ya kujiunga Mwaka 2006 akitokea Klabu ya Nchi kwao Legia Warsaw.
Licha ya kumtoa kwa Mkopo, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amedai Kipa huyo bado anaweza kuwa hazina kwao kwa vile atapata uzoefu zaidi huko Italy.
YOUNG KUTUA SPURS?
Winga wa Manchester United Ashley Young anavumishwa kutakiwa kwa udi na uvumba na Klabu ya London Tottenham Hotspur.
Ingawa habari hizi hazijathibitishwa, Spurs wamesemwa kuwa wanahitaji Winga ili kuziba pengo wanaloweza kuwa nalo ikiwa Mawinga wao kina Erik Lamela, Andros Townsend na Aaron Lennon, watahama kama pia inavyovumishwa.
Ripoti hizo zimedai Spurs inamwona Young, mwenye Miaka 30 na ambae amebakiza Mwaka mmoja tu kwenye Mkataba wake na Man United, kama mlengwa wao mkuu kutokana na Mchezaji huyo kukabiliwa na upinzani mkubwa kwenye nafasi yake huko Old Trafford.
Katika pozisheni ya Young huko Man United, Wachezaji wanaochipukia ambao wanamkosesha raha ni Mbrazil Andreas Pereira, Adnan Januzaj na Mchezaji mpya Memphis Depay huku pia upo uwezekano wa Muargentina Angel Di Maria kuleta upinzani ikiwa hatahamia PSG kama inavyosemwa.

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP