Posts

Showing posts from June, 2015

RAIS WA GAMBIA AONGEZEWA JINA JINGINE

Image
Rais wa gambia Yahya Jammeh Rais wa taifa la Gambia ambaye amekaa kwa kipindi kirefu madarakani Yahya Jammeh ameongezwa jina la Babili Mansa juu ya jina lake. Kulingana na kabila la Mandika jina hilo lina maana ya 'mtengezaji daraja mkuu' ama 'mshindi wa mito'. Taarifa kutoka kwa rais imesema kuwa rais Jammeh sasa anapaswa kuitwa mtukufu Sheikh Profesa Alhaji daktari Yahya AJJ Jammeh Babili Mansa. Alichukua jina hilo mara moja mwaka 2014 kabla kuliacha kulingana na ripoti. Rais Jammeh alichukua mamlaka mwaka 1994 alipokuwa luteni wa jeshi na amefanikiwa kushinda chaguzi 4 ambazo zimekosolewa mbali na kukabiliwa na majaribio kadhaa ya mapinduzi. Ameiambia BBC mwaka 2011 kwamba atatawala kwa miaka bilioni moja..iwapo Mungu atamruhusu. Iwapo ungependa kuongeza jina jingine juu ya jina lako basi ni jina gani ungependelea kupewa?

VICHWA VYA HABARI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 21,2015 VIKO HAPA

Image
                                                                     

Baraka Da Prince kutoa ngoma na Patoranking wa Nigeria

Image
Mwanamuziki bora Chipukizi anayeibukia kwenye game ya Bongo Flava Baraka Da Prince ambaye anatesa na ngoma yake Siachani Nawe amesema, lengo lake kwa sasa ni kuvuka anga la kimataifa. Baraka kijana toka jiji lenye mawe mengi Mwanza, alifunguka mengi pale alipokutana na mwandishi wetu, huku akiwashukuru wadau na mashabiki wake kwa kumfanya aweze kuibuka na tuzo ya Mwanamuziki bora Chipukizi anayechipukia, kwenye tuzo za muziki za kilimanjaro kwa mwaka 2014/2015. “Hii tuzo inanifanya nijiamini zaidi kwenye safari yangu ya kiinternational, na baada ya mwezi mtukufu kuna ngoma moja itatoka ambayo ni tofauti kabisa na nimemshirikisha mwanamke hatari sana itakua ni surprise kubwa”, alisema Baraka. Baraka aliweka wazi kuwa kimataifa ataanza kutoa ngoma na mkali toka nchini Nigeria Patoranking ambaye anatesa na ngoma yake ya Girlie. “Tukitoka Nigeria, watu wakae sawa kwani tunamalizia mazungumzo na Jaguar wa nchini Kenya ili tutoe ng...

Tazama hapa orodha ya nchi zenye amani duniani

Image
Taasisi ya uchumi na amani duniani imetoa orodha nzima ya nchi zenye amani duniani kwa kufuata vigezo mbalimbali.Vigezo hivyo ni pamoja na pamoja na vita vya mara kwa mara,mapigano ya hapa na pale na hali ya ugaidi kwa ujumla wake.Kwa kufuata vigezo hivyo utaina kuna nji zimefungana kwenye namba moja kwa sababu zimefanana kila kitu kwenye mahesabu yao.Nchi ya Iceland imeongoza kwa mwaka 2015 wakati huohuo nchi ya Syria imeshika mkia. Orodha kamili ni hii hapa chini; 1.Iceland 2.Denmark 3.Austria 4.New Zealand 5.Switzerland 6.Finland 7.Canada 8.Japan 9.Belgium 10.Norway 11.Czech Republic 11.Sweden 13.Ireland 14.Slovenia 15.Australia 16.Bhutan 17.Germany 18.Portugal 19.Slovakia 20.Netherlands 21.Hungary 22.Qatar 23.Poland 24.Mauritius 25.Singapore 26.pain 26.Croatia 28.Taiwan 29.Uruguay 30.Chile 31.Estonia 32.Bulgaria 32.Malaysia 34.Italy 35.Romania 36.otswana 37.Kuwait 37Laos 39.Latvia 40.United Arab Emirates SOMA: Nchi Duniani Ambazo Raia Wa Tanzania Haitaji Visa Kwenda.. 40.Mongoli...

simba yasaka makocha wa viungo

Image
SIMBA jeuri! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya klabu hiyo kumalizana na kocha kutoka Uingereza pamoja na wasaidizi wake wawili kutoka nchini humo ambao wote watatua nchini muda wowote kuanzia sasa. Simba imeona ni vema kuajiri makocha wenye kila aina ya ujuzi unaotakiwa katika klabu ya soka, akiwamo mtaalamu wa mazoezi ya viungo, ya uwanjani ya mambo ya mbinu na ufundi ambayo yatasimamiwa na kocha mkuu. Habari za ndani kutoka Simba zinasema tayari wamefanikiwa kuwapata makocha hao watatu ambao majina yao yatafahamika siku chache kabla ya kutua nchini tayari kuleta changamoto mpya ndani ya kikosi chao msimu ujao.

Abramovich Avuruga Mipango Ya Jose Mourinho

Image
Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich amevuruga mipango ya kocha Jose Mourinho ya kutaka kipa wao mkongwe, Petr Cech ahamie nje ya England. Badala yake, bilionea huyo wa Urusi ameamua kwamba Cech anayetaka kubaki London, akiwa na nia ya kukubali ofa ya Arsenal, aruhusiwe kutua Emirates. Mourinho alikuwa anataka Cech asiuzwe kwa wapinzani wao wanaowania nao ubingwa msimu ujao, bali aende klabu nyingine kama Paris Saint-Germain (PSG) waliokwishaonesha nia ya kutaka kumsajili. Watu wa ndani wa Chelsea wanasema kwamba Abramovich ameingilia kati mpango huo na kusema Cech aruhusiwe kwenda anakotaka, ikiwa ni kumpa heshima kwa kazi kubwa aliyowafanyia kwa miaka 11. Cech, 33, raia wa Jamhuri ya Czech alishaeleza nia yake ya kubaki London ambako familia yake imeshapazoea tangu 2004 aliposajiliwa kutoka Renes ya Ufaransa. Akiwa an Chelsea, Cech ameweka historia ya kuwa kwenye vikosi vilivyotwaa mataji yote ...

Wabunge wameitaka serikali kufanya uchunguzi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka.

Image
Baadhi ya wabunge wameitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina katika mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka-DART-kwa madai ya kuwepo kwa ufisadi mkubwa na uchotwaji wa mabilioni ya fedha ya ujenzi wa mradi huo. Akichangia maoni ya hotuba ya bajeti ya serikali ya mwaka 2015/16, mbunge wa viti maalum, Mhe Esther Matiko amesema barabara hiyo haina maeneo ya watembea kwa miguu, pikipiki, na upana wa barabara hiyo hauwezi kuruhusu malori mawili kupita kwa wakati mmoja na kusisitiza inaufisadi wa hali ya juu, huku mbunge wa Singida Magharibi akiitaka serikali kuhakikisha inafuatilia fedha katika benki ya Exim ili kutekeleza mradi wa umeme wa upepo ulioanza takribani miaka saba iliyopita.    Aidha, suala la ongezeko la tozo katika mafuta limechukua nafasi kubwa ya miongoni mwa wabunge katika mjadala wa hotuba ya bajeti kwa siku ya tano mfululizo ambapo mbunge wameendelea kuilalamikia serikali kwa kuweka tozo katika mafuta hususani ya taa na...

VICHWA VYA HABARI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI ,20,2015

Image