VAN GAAL KUONDOKA KWA SABABU YA MKE
Meneja
wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa huenda akaondoka
katika kilabu ya Manchester United mwisho wa kandarasi yake ya miaka
mitatu ili kutimiza ahadi aliyotoa kwa mkewe.
Alipoulizwa
iwapo ataongeza kandarasi yake kwenye klabu hiyo yenye maskani yake Old
Traford ,raia huyo wa Uholanzi ameiambia BBC kwamba ataondoka mwisho wa
kandarasi yake mwaka 2017.
''Nilimuahidi mkewe wangu.hatuna miaka mingi iliosalia,na hiyo ndio sababu'', alisema meneja huyo mwenye umri wa miaka 63.
''Nimefanya kila kitu katika maisha yangu kama mkufunzi''.
Alipulizwa
iwapo kuna uwezekano wa yeye kusalia katika klabu hiyo,alijibu kwamba
hawezi kutoa jibu lolote kwa kuwa mkewe amekasirika sana.
''Nakiri
kwamba nilimwambia kuwa ningestaafu ifikiapo miaka 55 lakini mapaka
sasa nikiwa na umri wa miaka 63 bado naendelea na ukufunzi na wiki ijayo
natarajia kufikisha miaka 64''alisema meneja huyo.

Comments
Post a Comment