HATMA YA BALOTELLI IPO HIVI KAMA ALIVYOSEMA BRENDAN RODGERS
Liverpool inasajili sana wachezaji hasa ambao
wanaocheza namba moja na Balotelli. Pia hivi
karibuni Balotelli alimtetea Raheem baada ya
kuhama Liverpool kwenda Manchester city na
mashabiki wa Liver walimshambulia Balotelli
kwenye mitandao.
Lakini Balotelli ameachwa kwenye pre season
kwasababu ya kufiwa na baba yake mlezi lakini hivi
sasa yupo kwenye mazoezi kwenye uwanja wa
Melwood.
Rogers alipoulizwa kuhusu hatma ya mchezaji huyo
alisema, “Mario hayupo kwenye tour yetu lakini
anafanya mazoezi kwa bidii na baadhi ya wachezaji
uwanjani. Sijui future yake iko vipi lakini ninavyojua
future yake ipo mikononi mwake kwa kufanya
mazoezi kwa bidii. Lakini najua anafanya kazi kwa
bidii kwa ajili ya kujiandaa kwa msimu ujao”
Namba ya Balotelli ipo kwenye ushindani mkubwa
baada ya usajili ambao Liverpool wameufanya na
ambao wanatarajia kuufanya kwa kutoa ofa ya
£32.5 million kumsajili Christian Benteke source shaffih dauda
Comments
Post a Comment