Tiger Woods -Sikuwa nimelewa kwa kunywa pombe
Mcheza gofu maarufu duniani Tiger Woods, amesema hakuwa amekunywa pombe alipokamatwa akiendesha gari jimbo la Florida mapema hapo jana. Mchezaji huyo alifunguliwa mashtaka ya kuendesha gari akiwa amelewa, lakini amesema ulevi wake ulitokana na dawa alizokuwa amezinywa kwa ushauri wa daktari. Polisi wa Palm Beach County,Forida, wamempiga picha akionekana kuwa mchovu na nywele zikiwa rafu. “Nafahamu uzito wa kitendo nilichokifanya na nawajibika kikamilifu na vitendo vyangu,” alisema. Polisi walitoa picha ya Bw Woods, akionekana kutokuwa nadhifu, nywele zake zikiwa hazijachanwa na macho akiwa ameyatoa nje na kuonekana mwenye uchovu. Alikamatwa katika mji wa Jupiter. “Nataka umma ufahamu kwamba pombe haikuhusika kwa vyovyote vile. Kilichotokea ni madhara ambayo hayakutarajiwa ya kutumia dawa kwa ushauri wa daktari,” alisema. “Sikugundua kwamba kuchanganya dawa kungeniathiri sana hivyo.” Aliongeza, “Ningependa kuomba radhi ...