Posts
Showing posts from April, 2016
Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP
- Get link
- X
- Other Apps
Klabu ya soka ya crystal Palace imetinga hatua ya Fainali ya FA CUP baada ya kuifunga Watford United Bao 2-1 kwenye Nusu Fainali. Kwa matokeo hayo ya mchezo huo uliochezwa Uwanjani Wembley, Jijini London, sasa Palace watakutana na Manchester United ambao waliwatoa Everton 2-1 katika Nusu Fainali nyingine. Hadi Mapumziko Palace walikuwa mbele kwa Bao 1-0 lililofungwa na Yannick Bolasie. Kipindi cha Pili, Watford walimudu kusawazisha kupitia Deeney lakini Dakika 6 tu baadae Connor Wickham akafunga Bao la Pili na la ushindi kwa Palace. Fainali Michuano hii itachezwa Mei 21 hapo hapo katika dimba laaWembley
Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo jumatatu April 25 2016
- Get link
- X
- Other Apps
Obama apinga mapinduzi ya kijeshi Syria
- Get link
- X
- Other Apps
Obama apinga kupindua serikali ya Syria Rais Barack Obama amesema kuwa, itakuwa ni makosa makubwa kwa mataifa ya Magharibi kutuma majeshi yake hadi nchini Syria ili kumuondoa madarakani rais wa Syria Bashar al-Assad. Akizungumza na BBC, Obama amesema itakuwa ni makosa makubwa kuwatuma wanajeshi wa nchi kavu nchini Syria kumpindua rais Assad kwa sababu hilo pekee halitasuluhusiha matatizo ya Syria. Rais huyo wa Marekani amerejelea maoni yake ya awali kuwa haina maana kwa makundi ya waasi kama vile Islamic State ndani ya Syria, kuendelea na makabiliano huku akisema kuwa jeshi la taifa hilo pekee lafaa kukomesha mapigano nchini humo. Ameongeza kusema hii itakuwa vigumu mno huku akiongeza kusema kuwa ni muhimu kuendelea kushambulia ngome za Islamic State ndani ya Syria kwa pamoja na kuzidisha juhudi za kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya muda mrefu nchini humo. Obama amesema itakuwa ni makosa makubwa kuwatuma wanajeshi wa nchi kavu nchini Syria kum...
Mwanamuziki Nguli,Papa Wemba afariki dunia.
- Get link
- X
- Other Apps
Mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia leo. Habari zinasema marehemu Papa Wemba amefia hospitali alikokimbizwa mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati akiwa katika onesho jukwaani. Papa Wemba alizaliwa June 14, 1949 huko Lubefu katika wilaya ya Sankuru nchini Congo. Alijipatia umaarufu sana kwa sauti nyororo na midundo ya Soukous ulimwenguni kote, ikiwamo Tanzania ambako amezuru mara kadhaa na kujizolea mashabiki wengi. amezuru mara kadhaa na kujizolea mashabiki wengi.
Balaa!maiti nyingine yazikwa, yafukuliwa
- Get link
- X
- Other Apps
Maiti ya Mariki Kimario juzi ilifukuliwa na baadaye kuzikwa upya sehemu nyingine katika tukio jingine la kuchukua kimakosa maiti hospitalini. Tukio kama hilo lililotokea takribani wiki mbili zilizopita kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wakati ndugu walipochukua mwili kimakosa na kwenda kuuzika Usangi mkoani Kilimanjaro kabla ya watu wengine kupewa maiti ambayo si yao walipoifuata hospitalini hapo na kuibua tukio hilo. Kutokana na tukio hilo MNH ililazimika kulipa gharama za mazishi kwa familia ambayo mwili wa ndugu yao ulizikwa na familia nyingine. Tukio hilo la juzi lilitokea mkoani Arusha ambako Jeshi la Polisi lililazimika kusimamia kufukuliwa kwa mwili huo kwenye Kijiji cha Elkisongo kilicho Kata ya Kidinga wilayani Arumeru. Katika tukio hilo, ndugu walioenda kuchukua maiti ya Leshai Ngoisaye, walipewa maiti ya Kimario na kwenda kuizika takriban kilomita 50 kutoka Arusha mjini. Miili hiyo ilikuwa imehifadhiwa Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru....
List ya wanamichezo 10 matajiri zaidi nchini Uingereza
- Get link
- X
- Other Apps
April 23 2016 gazeti la Rich Times imetoa majina ya wanamichezo 10 wenye mkwanja mrefu kwa mwaka 2016 ndani ya Uingereza pekee, katika list hii majina mengi yaliotawala ni wanasoka kasoro namba 2, 3 na 10 ndio sio wanasoka, namba 2 wapo wachezaji tennis Andy na Jamie Murray , namba tatu yupo mchezaji golf Rory McIlroy huku namba 10 yupo bondia pekee Amir Khan . Mwanamichezo tajiri kwa mwaka 2016 ni nahodha wa Man United Wayne Rooney ambaye ana utajiri wa pound milioni 82 ambazo ni zaidi ya bilioni 250, utajiri wa Rooney unatajwa kuongezeka kwa kiasi cha pound milioni 10 wakati bondia Amir Khan kiwango chake hakijaongezeka wala kupungua.