TARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kupitia taarifa hii kwa vyombo vya habari, tunapenda kuutaarifu umma wa Watanzania wote nchini kuwa Mgombea Urais wa CHADEMA anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Mh. Edward Ngoyai Lowassa atahutubia taifa kupitia vituo mbalimbali vya televisheni, redio na njia zingine za upashanaji habari hususan mitandao ya kijamii (live streaming facebook, twitter, forums etc), siku ya Ijumaa, tarehe 23 Oktoba, 2015, saa 3 usiku. Kupitia hotuba hiyo kwa taifa, Mh. Lowassa atazungumza na Watanzania wote, ndani na nje ya nchi, na watu wa mataifa yote, kuhusu Tanzania mpya itakayotokana na MABADILIKO makubwa ya kimfumo, kiutawala na utendaji wa serikali atakayoiunda baada ya Watanzania kumpatia dhamana ya kuwa Mkuu wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu na Kiongozi Mkuu wa Serikali hapo Oktoba 25, 2015. Aidha, Mhe. Lowassa atatumia muda huo kuwashukuru Watanzania wote kwa namna walivyomuunga mkono kwa upendo mkubwa yeye...