Drogba kucheza na Lampad ligi moja marekani
I
Didier Drogba mwishowe akamilisha uhamisho wake kwa Impact de Montreal
Impact de Montreal siku ya Jumatatu ilitangaza kuwa imekamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba.
Staa wa Ivory Coast alikuwa bila klabu baada ya kuondoka Chelsea mwezi Mei, lakini sasa ataungana na mchezaji mwenzake wa zamani Frank Lampard katika Ligi ya Marekani.
"Ni heshima kumkaribisha Didier Drogba kwa Impact," Rais wa Montreal Joey Saputo aliiambia tovuti rasmi ya klabu.
"Kutokana na mazungumzo ya awali tuliyofanya naye, nilihisi kwamba kwa kweli alikuwa anataka kucheza katika Montreal. Hii ni moja ya siku kubwa katika historia ya klabu na itakuwa ya manufaa katika nyanja zote."
Drogba alicheza mechi 381, na kushinda mataji manne ya Ligi Kuu ya Uingereza katika awamu mbili akiwa na klabu hiyo ya London.

Comments
Post a Comment