Posts
Showing posts from August, 2016
Thierry Henry Kuwa Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji Kuungana na Roberto Martinez
- Get link
- X
- Other Apps
Kocha mpya wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez amesema mchezaji wa zamani wa klabu za Arsenal na Barcelona, Thierry, ambaye aling’aa sana wakati akichezea timu ya taifa ya Ufaransa, atakuwa mmoja wa wasaidizi wake. Henry alikuwa mmoja wa wakufunzi wa timu ya vijana Arsenal lakini akajiuzulu Julai baada ya meneja Arsene Wenger kumwambia kwamba hawezi kufanya kazi hiyo akiwa bado anaendelea kuwa mchanganuzi wa soka kwenye runinga. Wakati wa Euro 2016 Henry alikuwa akifanya kazi ya kuchambua soka katika vituo vya Sky Sports na pia alifanya kazi na BBC Sport. Thierry Henry alikuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1998 nyumbani.
Isome hii mpya ya MO DEWJI na SIMBA
- Get link
- X
- Other Apps
Mkurugenzi Mtendaji na rais wa makapumni ya Mohammed Enterprises Ltd (MeTL Group) Mohammed Dewji ‘MO’ ametoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa klabu ya Simba kwa ajili ya kusaidia zoezi la usajili kama alivyoahidi siku chache zilizopita. Bilionea huyo ambaye anania ya kuwekeza bilioni 20 alisema, yuko tayari kusaidia zoezi la usajili endepo klabu hiyo ingeridhia kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu kutoka wanachama wa kadi hadi kuwa kampuni ambayo itaendesha kwa mfumo wa kibiashara. Julai 31 klabu ya Simba iliridhia kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji japo haikujulikana mara moja kwamba wameamua kuingia katika mfumo upi. MO amesema ametimiza ahadi aliyoitoa baada ya wanachama wa klabu ya Simba kukubali kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji: “Niliahidi kusaidia kwenye zoezi la usajili kwa ajili ya klabu yetu ya Simba SC, ninafuraka kubwa sana kumkaribisha rais wa klabu (Simba). Mimi kama mwanachama ningependa kuchangia kwenye hilo zoezi.” Rais wa Simba Ev...