Arsene Wenger anafikiria kuhusu kustaafu? Huwa inamjia akilini, alafu…

Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene
Wenger amedumu na klabu ya Arsenal kwa zaidi ya
miaka kumi na tano toka alipojiunga nayo 1996,
Wenger anakuwa kocha wa pili katika historia ya
Ligi Kuu Uingereza kudumu na timu kwa muda
mrefu baada ya kocha wa zamani wa Manchester
United Sir Alex Ferguson ambaye amestaafu
mwaka 2013. Kufuatia kustaafu kwa Sir Alex Ferguson mwaka
2013 kumekuwa na maswali mengi kuhusiana na
Wenger lini atastaafu, wengi wanaamini Wenger
alikuwa na uwezo wa kuifundisha Arsenal kutokana
na rekodi alioweka ndani ya miaka tisa ya mwanzo
klabuni hapo, Wenger alishinda mataji 7 lakini
miaka kumi baadae Wenger ameishia kutwaa
mataji mawili pekee rekodi inayotia mashaka na
uwezo wake.
Wengi walitazamia kuwa kuna uwezekekano wa
Wenger kustaafu kwa miaka ya hivi karibuni lakini
alichojibu kuhusu suala la yeye kustaafu bado
linawaacha watu njia panda ya lini atastaafu.
“Kustaafu? ndio wakati mwingine huwa inanijia
akilini lakini sio zaidi ya sekunde 5 kwa sababu
huwa nahofia”>>> Wenger
“Nataka nifanye vizuri na klabu ili siku
nitakapoondoka naicha klabu katika nafasi nzuri ili
iweze kuendelea na kuendelea” Wenger

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP