Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP

Klabu
ya soka ya crystal Palace imetinga hatua ya Fainali ya FA CUP baada ya
kuifunga Watford United Bao 2-1 kwenye Nusu Fainali.
Kwa
matokeo hayo ya mchezo huo uliochezwa Uwanjani Wembley, Jijini London,
sasa Palace watakutana na Manchester United ambao waliwatoa Everton 2-1
katika Nusu Fainali nyingine.
Hadi Mapumziko Palace walikuwa mbele kwa Bao 1-0 lililofungwa na Yannick Bolasie.
Kipindi
cha Pili, Watford walimudu kusawazisha kupitia Deeney lakini Dakika 6
tu baadae Connor Wickham akafunga Bao la Pili na la ushindi kwa Palace.
Comments
Post a Comment