Obama apinga mapinduzi ya kijeshi Syria
Obama apinga kupindua serikali ya Syria
Rais
Barack Obama amesema kuwa, itakuwa ni makosa makubwa kwa mataifa ya
Magharibi kutuma majeshi yake hadi nchini Syria ili kumuondoa madarakani
rais wa Syria Bashar al-Assad.
Akizungumza
na BBC, Obama amesema itakuwa ni makosa makubwa kuwatuma wanajeshi wa
nchi kavu nchini Syria kumpindua rais Assad kwa sababu hilo pekee
halitasuluhusiha matatizo ya Syria.
Rais
huyo wa Marekani amerejelea maoni yake ya awali kuwa haina maana kwa
makundi ya waasi kama vile Islamic State ndani ya Syria, kuendelea na
makabiliano huku akisema kuwa jeshi la taifa hilo pekee lafaa kukomesha
mapigano nchini humo.
Ameongeza
kusema hii itakuwa vigumu mno huku akiongeza kusema kuwa ni muhimu
kuendelea kushambulia ngome za Islamic State ndani ya Syria kwa pamoja
na kuzidisha juhudi za kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya muda
mrefu nchini humo.
Obama
amesema itakuwa ni makosa makubwa kuwatuma wanajeshi wa nchi kavu
nchini Syria kumpindua rais Assad kwa sababu hilo pekee halitasuluhusiha
matatizo ya kisiasa ya Syria.
Obama
amesema itakuwa ni makosa makubwa kuwatuma wanajeshi wa nchi kavu
nchini Syria kumpindua rais Assad kwa sababu hilo pekee halitasuluhusiha
matatizo ya kisiasa ya Syria.
Katika
mahojiano ya kina, Bw Obama amesisitiza hitaji lake kuwa matatizo ya
kimataifa inahitaji uwajibikaji wa muda baada ya muda.
Obama
anasema kuwa itakuwa vigumu kwa majeshi yake ama hata muungano
unaongozwa na Marekani kuitokomeza kabisa Islamic State katika kipindi
cha miezi 9 za uongozi wake.
Cha mno anasema ni kudidimiza maeneo inayokalia IS na kushambulia ngome zake.
Aidha Obama anasema mashambulizi yatalenga haswa kukatiza msururu wa wapiganaji wanaoenda ulaya na kusababisha maafa makubwa.
Comments
Post a Comment