IGP SIMON SIRRO AFANYA ZIARA KISIWANI PEMBA
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akimsikiliza Mkuu wa mkoa
wa Kaskazini Pemba Omar Athuman (aliyesimama), wakati akitoa neno Mbele
ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Kaskazini na Kusini
Pemba, IGP Sirro yupo kisiwani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la
kujitambulisha na kuzungumza na watendaji wa Jeshi hilo.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akipokea salamu ya heshima
ya kijeshi kutoka kwa Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakati
akiwasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mkoa wa Kusini Pemba leo, IGP
Sirro yupo kisiwani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la
kujitambulisha na kuzungumza na watendaji wa Jeshi hilo.
Comments
Post a Comment