Majibu ya ukimya wa mchizi MOX

Mchizi Mox asema kuna mambo anafanya ndiyo maana anaonekana kama anafanya muziki kwa kurelax

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Mchizi Mox amefunguka na kuzungumzia kwanini anaonekana anafanya muziki kwa kurelax.

Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Mchizi Mox amesema kuna mambo mengi anafanya nje ya muziki ndiyo maana amekuwa akionekana kama anafanya muziki kwa relax. “Unajua zamani muda wangu wote nilikuwa nautumia kwenye muziki, sasa hivi nimekuwa mtu nzima, kuna majukumu yameonyezeka,” alisema Mox. “Lakini kitu kingine sasa hivi nafanya muziki wa meseji, sasa hivi ukisema nipige ngoma kama 'Watu Kibao' watu watacharuka, maisha yamebadilika kwa namna moja hata kwa aina ya muziki ambao jamii unauhitaji,” Aliongeza, “Kwa hiyo muziki wangu kwa sasa ni kila baada ya miezi mitatu. Pia nyimbo zangu hazifanani na za watu wengine, watu wengine wanaweza kutoa nyimbo kila mara kwa sababu meseji wamazoimba hazichelewi kufa, lakini mimi ni msanii ambae nikitoa kazi yangu sitaki ifanane na nyingine,” Rapa huyo anajipanga kuachia kazi yake mpya 'Oya Oya', ambapo amedai katikati ya mwezi huu itakuwa imetoka.

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP