Picha za uchache wa mashabiki wa arsenal kwenye mechi dhidi ya West brom
Yaliyoikuta Manchester United ilipokuwa ikicheza dhidi ya Crystal Palace yametokea kwenye uwanja wa Emirates usiku wa Alhamisi wakati Arsenal Ikicheza dhidi ya West Brom ambapo uwanja mashabiki wengi wa Arsenal hawakujitokeza uwanjani kushuhudia mchezo huo kama ilivyo kawaida yao.
Takwimu zilizotolewa na maofisa wa timu hiyo zinasema kulikuwa na watazamaji wapatao 59,000 wakati uwanja wao unauwezo wa kubeba mashabiki 60,432 lakini takwimu za viongozi hao ni kwa mujibu wa tiketi zilizouzwa na siyo watu walioingia uwanjani kushuhudia mtanange huo.
Uamuzi wa mashabiki kutoingia uwanjani ni moja kati ya shinikizo la kutaka uongozi wa timu hiyo kumtimua Arsene Wenger katika kikosi cha The Gunners kutokana na kushindwa kutwaa taji la VPL kwa muda mrefu pamoja na kuishia kwenye hatua ya 16 bora mara sita mfululizo kwenye michuano ya mabingwa Ulaya.
Lakini mgomo huo haukuiathiri timu ndani ya uwanja kwasababu iliwachukua dakika sita tu Arsena kupata bao lilifungwa na Alexis Sanchez aliyeachia shuti akiwa nje ya box.
Dakika ya 38 Sanchez aliifungia Arsenal bao la pili kwa mkwaju wa adhabu ndogo goli lililoipa timu yake pointi tatu na kujikita katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa pointi tano nyuma ya Spurs iliyonafasi ya pili kwenye msimamo wa EPL.



Comments
Post a Comment