Maneno y kocha Mayanja kuhusu ubingwa VPL

Kocha
wa vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, Wekundu Wa Msimbazi Simba,
Jackson Mayanja amesita kuzungumzia suala la ubingwa licha ya kikosi
chake kuonyesha dhamira ya kuuwania kwa msimu huu.
Mayanja
amesita kulizungumza suala hilo, baada ya kuulizwa kama ana uhakika wa
kuirejesha heshima ya ubingwa Msimbazi, ambayo imepotea kwa zaidi ya
miaka minne sasa.
Kocha
huyo kutoka nchini Uganda, amesema ni mapema mno kuzungumza suala la
ubingwa ambao pia unapigiwa upatu na klabu nyingine mbili za Young
Africans pamoja na Azam FC.
“Ukiuzungumzia
ubingwa kwa sasa utakuwa unajidanganya kwa sababu hao tuanofukuzana nao
pia wapo katika hali nzuri, kwa hiyo yeyote anaweza kuuchukua”.
“Ukiangalia
hali ilivyo utaona kabisa kwamba Yanga na Azam kwa alama walizonazo pia
wanaweza kumaliza katika nafasi ya kwanza, hivyo ukinitaka mimi niseme
kama Simba itakuwa bingwa au la, nitashindwa kukuhakikishia hilo,
Alisema kocha Mayanja.
Comments
Post a Comment