Unajua Messi kapiga chini Ofa ngapi za Real Madrid? Jibu hili hapa

Mara ya mwisho kwa Real Madrid kumsajili mchezaji kutoka kwa mahasimu wao Real Madrid ilikuwa mnamo mwaka 2000 – wakati Luis Figo alipojiunga na Madrid kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi wakati huo – uhamisho ulikuza uhasama baina ya vilabu hivyo na tangu wakati huo hakujawahi kutokea biashara baina yao.
  Sasa takribani muongo mmoja upite tangu walipomchukua Figo Camp Nou – Real Madrid wamekuwa wakijaribu kwa nguvu zote kumsajili staa wa FC Barcelona, Lionel Messi, imeripotiwa.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Spain likiwemo gazeti la Cope – vimeripoti kwamba mshindi wa mara tano wa tuzo ya Ballon D’Or Lionel Messi, 28, amekuwa akipata maombi ya Madrid kujiunga nao lakini amekuwa akizipiga chini ofa za Los Blancos.
Ripoti zinasema kwamba ofa ya kwanza ilitumwa mwaka 2011 wakati Real walipokuwa na hofu kwamba staa wao Cristiano Ronaldo alikuwa njiani kuelekea Man City.
Real wakarudi tena mara ya pili wakati kiongozi wa juu wa klabu hiyo ambaye jina lake halikutajwa alipofanikiwa kukutana na Messi lakini jibu la Lionel likawa lile lile kwamba angependa kubaki na La Blaugarana.
Jaribio la 3 la Madrid lilikuja mwaka uliopita kiongozi huyo huyo wa Madrid alipojaribu tena kuongea na Messi lakini akagonga mwamba kumshawishi Muargentina huyo.
  Baada ya Messi kupiga chini ofa 3 – inawezekana ndio maana Real wamegeuzia malengo yao kwa Neymar katika siku za hivi karibuni.
Florentino Perez inasemekana anapoteza uvumilivu na tabia za Ronaldo kusafiri ovyo na hivyo kupelekea kiwango chake kuporomola na sasa anatafuta mbadala wake.
CREDIT TO 
SHAFFIH DAUDA

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP