Unajua wachezaji wenye kasi zaidi uwanjani ulimwengun
Licha
ya kuwa mchezo wa soka unahitaji ubunifu maarifa na ufundi, kasi pia ni
moja kati ya kitu kinachomuongezea thamani mchezaji, kuna baadhi ya
namba uwanjani huhitaji wachezaji wenye kasi zaidi. Kama ambavyo kwa
Tanzania Mrisho Ngassa anatajwa kuwa na kasi, kiasi hata cha mkenya
McDonald Mariga kumsifia, ila wapo wachezaji wengine wanaotajwa kuwa na
kasi zaidi duniani. Hadi kufikia mwezi Mei 2015, hii ndio ilikuwa 'Top
5' ya wachezaji soka wenye kasi zaidi duniani, stori kutoka
talksport.com
5-
Theo walcott ni moja kati ya mastaa wa soka wa Uingereza wenye kasi
zaidi duniani,Walcott kwa mujibu wa talksport.com anatajwa kuwa na uwezo
wa kukimbia Kilometa 32.7 kwa saa.

4-
Staa wa soka wa klabu ya Real Madrid ya Hispania na timu ya taifa ya
UrenoCristiano Ronaldo anatajwa kuwa na uwezo wa kukimbia kwa kasi ya
Kilometa 33.6 kwa saa. Uwezo ambao unamfanya aingie katika list ya
mastaa watano wenye kasi zaidi duniani.

3-
Aaron Lennon licha ya kuwa katika list ya wachezaji wafupi zaidi
wanaocheza Ligi KuuUingereza Aaron Lennon yupo katika Top 5 ya mastaa
wenye kasi zaidi uwanjani.Lennon anatajwa kuwa na uwezo wa kukimbia
Kilometa 33.8 kwa saa.

2-
Gareth Bale inatajwa ni nadra sana kumkosa staa huyu katika Top 5 hii,
kwani amewahi kuingia katika headlines za kumzidi mbio moja kati ya
mabeki bora dunianiMaicon. Hivyo ni nadra sana kukosekana katika
headlines za mastaa wenye kasi zaidi.Bale anatajwa kuwa na uwezo wa
kukimbia kwa kasi ya Kilometa 34.7 kwa saa.

1-
Antonio Valencia ni staa wa soka kutokea Ecuador, anatajwa kuwa na
uwezo wa kucheza nafasi mbili kwa ufasaha uwanjani, kama winga wa kulia
na beki wa kulia, Valencia ambaye anakipiga katika klabu ya Manchester
United ya Uingerezaanatajwa na mtandao wa talksport.com kuwa mchezaji
kasi zaidi duniani, ana uwezo wa kukimbia kwa kasi ya Kilometa 35.1 kwa
saa.

Credit:Millard Ayo
Comments
Post a Comment