RONALDO AMZUNGUMZIA MAMA WA MWANAE PAMOJA NA KURUDI MAN UNITED

Ronaldo amesema hatomtaja mama wa mtoto wake mpaka atakapoona muda umefika
Ronaldo amesema hatomtaja mama wa mtoto wake mpaka atakapoona muda umefika
Mchezaji Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, amesema kamwe hatomtaja mama mzazi wa mtoto wake Ronaldo Jr. na kwamba muda ukifika atamuweka wazi huku mwanae pia akitakiwa kusubiri muda muafaka apate kumjua mama yake.
Amesema kuwa amekua akishiriki mapenzi na warembo tofauti tofauti huku akikiri kuwa hiyo sio yeye tu bali ni tatizo kwa nyota wengi duniani kupitia maisha hayo huku akijinasibu kuwa kwasababu yeye ni mrefu, mwenye mwili mzuri wa mazoezi basi huwamaliza akina dada.
Ronaldo ameweka wazi maisha yake binafsi wakati akifanyiwa mahojiano na Jonathan Ross
Ronaldo ameweka wazi maisha yake binafsi wakati akifanyiwa mahojiano na Jonathan Ross
Kuhusu Balon d’Or msimu huu, Ronaldo anasema Messi atatwaa tuzo hiyo kutokana na klabu yake ya Barcelona kutwaa makombe yote matatu iliyoshiriki msimu uliopita. Huku Ronaldo akisema ulikua ni msimu mzuri zaidi kwake binafsi kutokana na kufunga magoli mengi katika kila mashindano.
Ronaldo ambaye alikua jijini London kwa utambulisho wa filamu yake ya maisha yake ya soka, anasema kamwe hatarajii kustaafu hivi karibuni huku akisema atamaliza mpira wake katika ligi bora na sio Marekani wala Qatar. Huku akisema lolote linawezekana kwa yeye kirejea Manchester United siku moja na kwamba tusubiri kuona.
Mchezaji wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo aliachana na penzi wake wa zamani Irina Shayk baada ya kudumu kwenye uhusiano kwa miaka mitano
Mchezaji wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo aliachana na penzi wake wa zamani Irina Shayk
aada ya kudumu kwenye uhusiano kwa miaka mitano
source shaffih dauda.com

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP