TIFFAH alivyopokelewa kwa furaha na familia ya Zari huko Afrika Kusini.

Pamoja na kuwa ni watoto wa baba tofauti, watoto wa kiume wa Zari wamempokea kwa furaha kubwa Tiffah, mtoto wa Zari the Bosslady. 
Zari kwenye picha hii ameandika: If anybody ever said perfect doesn’t exist, they were wrong. It surely does!!!! Look at my ‘perfect’ lil life 
Baada ya Tiffah kufikisha siku 40, sasa ni muda wa kuonana na kaka zake hao watatu wanaoishi nchini Afrika Kusini. 
Mrembo huyo wa Uganda mwenye makazi yake South ameendelea kushea picha zinazowaonesha wanae wakicheza kwa upendo mkubwa na mdogo wao Tiffah. 
Katika picha nyingine aliyoshea jana Zari aliandika, “Someone didn’t move an inch… spent half of his night just staring,” ameandika Zari kwenye picha hiyo. 
Zari na Tiffah walielekea Afrika Kusini wiki hii baada ya kukaa Tanzania kwa kipindi cha miezi takriban mitatu tangu akiwa mjamzito. 
Tiffah akifurahia usingizi kwenye ndege wakati yeye na mama yake wakiwa safarini Afrika Kusini

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP