Maamuzi ya UKAWA baada ya chama pinzani kukiuka taratibu za kisheria…


Suala la uchaguziMkuu bado linagonga vichwa vya habari hapa nchini ambapo Mwanasheria wa CHADEMA ambaye ni mkuu wa idara ya Uchaguzi kwenye sheria,Bw.John Mallya jana alifanya mkutano wa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu uki ukwaji wa sheria na chama pinzani.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Mallya alisema: "Ndugu waandishi wa habari tumewaita hapa hususani mambo ya kisheria yanayoendelea kwenye kampeni zoezi la uchaguzi ni zoezi la kikatiba, sheria ya uchaguzi wa taifa mwaka 1985 kanuni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na maadili ya uchaguzi wa Ubunge, Urais na Udiwani pamoja na sheria nyingine ikiwemo ya rushwa na sheria ya vyama vya kisiasa".

‘Sheria kwa mfano, ambayo ni maadili ya Uchaguzi ya mwaka huu vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huu kupitia makatibu wake wakuu wameweka saini zao inakataza suala la mtu kutoa bango la mtu mwingine lakini chadema imepata hiyo changamoto kwamba mabango yake wameondolewa kwa mfano hili bango lipo Nyerere Road pale Mwanza limeondolewa na watu wa CCM ilikuwa ni nyumba ya mtu binafsi wakamtishia watachoma nyumba yake wakamrushia mawe wakavunja vioo vyake na baada wakaliondoa"

‘Na hii inaonesha sio tu ni namna gani CCM wamekiuka sheria lakini hawafai kutawala nchi kwasababu suala la kuweka bango ni suala la kisheria ukiona bango la Samia,Magufuli na mtu yoyote limewekwa kisheria", aliongeza Mallya.

‘Mabango, sera, vipeperushi vyote vinakuwa vimesajili na tume ya Uchaguzi kwa madhumuni ya Kampeni kwa mfano ujumbe wa Mabadiliko umesajiliwa na nembo ya CHADEMA pia imesajiliwa, sasa CCM wanakiuka sheria wamekopi na kupesti, wanachukua ilani na sera zetu ambapo wamechukua nembo yetu M4C ambayo sisi tunaita Movement 4 Change huku CCM wakiwa wanasema M4C ni Magufuli 4 Change‘ – John Mallya

‘Katika hili tumechukua hatua nzito kuliko hizi za mwanza maana yake hili sio la kimadili hili ni uvunjwaji wa sheria, Chadema tunampeleka Magufuli Mahakamani pamoja na bodi ya wadhamini wa chama cha Mapinduzi", alisema.

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP