Kwanini wenger haja sajili mshambuliaji msimu huu ? majibu ni haya
Arsenal
hawana tatizo la katika safu yake ya ushambuliaji, hayo ni maneno ya
Arsene Wenger ambaye pia anasema uwepo wa Alexis Sanchez, Olivier Giroud
na Theo Walcott, unaweza kumpa magoli zaidi ya 20 kwa msimu.
Arsenal
walihusishwa na usajili wa Karim Benzema na Edinson Cavani, lakini hata
hivyo mambo yalikwenda ndivyo sivyo na badala yake kuamua kutonunua
mshambuliaji yeyote.
“Nadhani Giroud, Walcott na Sanchez wanaweza kuleta magoli zaidi ya 20 bila tatizo lolote lile", aliwaambia waandishi.
"Wakati
mwingine lazima uwaamini wachezaji wako na kuwapa nafasi. Halafu baada
ya muda watafanya vyema tu. Mara nyingi watu hutaka mafanikio ya haraka,
lakini hatuendi hivyo.
“Nina
Aaron Ramsey ambaye anaweza kufunga magoli 15, Mesut Ozil 15, Santi
Cazorla 10. Vinginevyo, kama una mchezaji mmoja ambaye ndiye unategemea
kwa ufungaji, siku akipata majeraha je?, nani atafunga sasa”.
Wenger
amekosolewa kwa kutosajili mshambuliaji mpya katika dirsha la usajili
lililofungwa mapema mwezi huu, lakini alilisisitiza kuwa kwa sasa
washambuliaji hawapatikani tena katika bara la Ulaya.
"Washambuliaji wengi wanapatika nara la Amerika ya Kusini kwa sasa. Bara la Ulaya hawazalishi washambuliaji siku kabisa.
"Angalia
nchi kama Ujerumani, ambayo ilicheza dhidi ya Scotland au dhidi ya
Poland huku Mario Gotze ndio akiwa mshambuliaji wa mwisho – huyu ni
kiungo. Si kana kwamba hawataki kumchezesha mshambuliaji halisi pale
mbele lakini hayupo mshambuliaji ambaye ana vigezo vya kusimama pale
mbele.
"Nani ambaye unamuona hapa Ulaya?"
"Kitu
ninachoweza kusema ni kwamba, katika hizi akademi za soka zinatakiwa
kuwatenegeneza washambuliaji tangu wakiwa katika umri mdogo. Kuna umri
kati ya miaka mitano mpaka 12 ambapo ndipo unaweza kutengeneza kipaji
cha maana. Umri katika ya miaka 12-14 unaanza kumtengeza katika kasi
yake na nguvu katika mwili.

Comments
Post a Comment