Jinsi yanga walivyo jipanga kuwakabili simba kesho katika VPL
YANGA
inaendelea na mazoezi yake hapa kisiwani Pemba, tayari kwa kuwavaa
watani wao Simba kesho Jumamosi, lakini katika mazoezi yao ya juzi jioni
na jana Alhamisi makocha Hans Pluijm na Boniface Mkwasa walifanya zoezi
moja kubwa la kukaba tu na kushambulia.
Katika
mazoezi yao yanayofanyika katika Uwanja wa Gombani, Pluijm na Mkwasa
waligawanya vikosi vitatu vilivyokuwa vikipishana kila baada ya dakika
15 ambapo kila mchezaji alitakiwa kumkaba mwenzake zoezi lililoashiria
ukabaji unaohitajika Jumamosi.
Mkwasa
ndiye aliyekuwa msimamizi mkuu katika zoezi hilo, ambapo alikuwa mkali
kila alipokuwa akimuona mchezaji yeyote akifanya uvivu wa kukaba huku
mara unapopata mpira jukumu la kushambulia linaanza mara moja.
MATTEO AKIONA
Zoezi
hilo liliendana na adhabu mbalimbali kwa waliofanya uzembe na straika
Matteo Simon alikumbana na adhabu ya kupiga ‘pushapu’ 15 baada ya
kuzembea kukaba Oscar Joshua aliyekwenda kufunga kirahisi bila ya
kukabwa na mshambuliaji huyo.
Uchuguzi
wa Mwanaspoti umebaini kwamba kufanyika kwa zoezi hilo makocha hao
waligundua udhaifu wa kikosi chao katika kukaba kwa nguvu mara
wanapopoteza mpira kitu abacho kingeweza kuwapa madhara katika mchezo
dhidi ya Simba.
COUTINHO AMSHTUA PLUIJM
Ishara
ya kuingia kwa dozi hiyo ni kitendo cha kukaba kwa nguvu kwa kiungo
Andrey Coutinho ambaye alikabidhiwa kukabana na Yondani, ambapo wakati
Yondani akienda kufunga Coutinho licha ya kuonekana yuko hoi alikimbia
na kumpokonya mpira beki huyo kitu ambacho kilimvutia Pluijm na
kumpongeza wa kumtamkia; “Vizuri Coutinho leo umefanya kitu ambacho
sijawahi kukiona tangu nimekujua, safii”.
WAJAZWA PUMZI
Achana
na zoezi hilo la juzi kabla ya mazoezi hayo katika mazoezi ya siku ya
Jumanne kikosi Pluijm na Mkwasa nusura wapasue mapafu ya wachezaji hao
baada ya kuwakimbiza kwa muda mrefu.

Comments
Post a Comment