VERMAELEN APELEKA USHINDI BARCELONA

MABINGWA watetezi, Barcelona wamepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Malaga Uwanja wa Camp Nou katika mchezo wa La Liga.
Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee, beki Mbelgiji Thomas Vermaelen dakika ya 73. Mbelgiji huyo alikuwa nje kwa majeruhi karibu mwaka mzima msimu uliopita baada ya kusajiliwa kutoka Arsenal.
Luis Suarez, Lionel Messi na Neymar wote walianza katika safu ya ushambuliaji, lakini hakuna kati yao aliyefumga. 
Kikosi cha Barcelonakilikuwa Bravo; Sergi Roberto, Mascherano, Vermaelen, Alba/Mathieu dk89, Busquets, Rakitic/Rafinha dk64, Iniesta, Messi, Suarez na Neymar/Sandro dk85.
Malaga; Kameni; Rosales, Angeleri, Weligton/Albentosa dk25, Torres, Horta, Tissone, Recio; Juankar, Amrabat/Charles dk53

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP