Mourinho ana wasiwasi na Giego Costa
kocha wa Chelsea Jose Mourinho anasema kuwa anakuwa na wasiwasi kuhusu uhodari wa Diego Costa kabla ya kuanza Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Swansea.
Costa ambaye aliumia katika maandalizi ya Community Shield ambapo Chelsea walipigwa bao 1-0 dhidi ya Arsenal.
"Wiki iliyopita hakuweza kucheza katika Community Shield. Hakukuwa tayari kushiriki,'' Mourinho aliwaambia watangazaji habari katika uzinduzi wa Ligi Kuu ya Uingereza.
"Siwezi kuwahakikishia mashabiki kuwa ataendelea kuwa bora lakini naweza kuwahakikishia kuwa anafanya kazi vizuri na kwa bidii na kila mtu karibu naye anamsaidia.
"Sipendi kulia au kuguna kuhusu wachezaji ambao hawachezi. Lakini ni dhahiri katika kikosi kidogo kama hiki tunacho, basi wakati mtu anakosekana sifurahi. Lakini sitakuwa na sababu. "
Costa alifunga mabao 20 katika mashindano yote kwa Chelsea msimu uliopita, lakini alikumbana na tatizo la kupata jeraha katika kipindi cha pili cha kampeni.
Comments
Post a Comment