maneno ya wenger kwa mourinho baada ya ushindi wa jana dhidi ya chelsea

Arsene Wenger amepata nafasi ya kukataa wazo la Jose Mourinho kuwa Arsenal waliacha falsafa yao kwa makusudi ya kuwapiga Chelsea katika Community Shield siku ya Jumapili katika Wembley.
Kocha Mreno aliwapongeza Arsenal baada ya mchezo lakini alimlaumu mwenzake Arsene Wenger kwa 'kuacha falsafa yake katika chumba cha kuvalia.
"Kwa maoni yangu ni timu inayolinda vizuri sana, ambayo inaacha falsafa yake katika chumba cha kuvalia, inabadilisha mtazamo wake, inatumia wachezaji tisa katika kipindi cha pili chote katika boksi, haifungwi na inafunga bao moja, kutokana na mtazamo huo wanastahili kushinda, "Mourinho aliwaambia watangazaji habari.
"Hii ni soka. Huu ni mfumo mzuri. Hongera kwao."
Kwa upande mwingine, akizungumza na watangazaji habari, Wenger alijibu: "Sisi hatukuachilia kitu. Tulilinda vizuri. Mchezo wetu ni kuweka pamoja, kwa mshikamano, na kulinda na kushambulia vizuri.
Chelsea  wataanza kutetea taji lao la Ligi Kuu wakikaribisha Swansea Jumamosi ijayo, wakati Arsenal itamenyena na West Ham siku hiyo hiyo katika Emirates Stadium.

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP