Kutana na beki ambaye Neymar ana muogopa



mchezaji staa wa brazil Neymar jr amemtaja Sergio Ramos kuwa ni moja ya mabeki visiki kabisa aliowahi kukutana nao katika maisha yake ya soka.
Nyota huyo wa Barcelona amemuelezea mlinzi huyo wa kati wa Real Madrid kama " beki kisiki" wakati alipokuwa akiulizwa ni beki gani ambaye anahisi humletea shida katika maisha yake ya soka.
Lakini hata hivyo Neymar pia amesema wachezaji wenzake Javier Mascherano na Gerard Pique pia humpa shida wakati wakiwa mazoezini bila ya kusahau Mbrazil mwenzake Thiago Silva.
"Ni vigumu kusema kuhusu hili, kuna mabeki wengi sana wa kiwango cha juu" alisema. "wapo kina Mascherano, Pique, Thiago Silva ila Sergio Ramos - ni beki wa kati bora sana".
 
 Neymar reveals the toughest defenders and best goal of his career

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP