kuhusu wapinzani wake kufanya usajili wa kufa mtu, huku yeye akiwa bado anapepesa, hii ndio kauli ya Mourinho
Kocha
wa Chelsea Jose Mourinho hatetemeshwi na hali ya klabu yake kutofanya
usajili wa nguvu mpaka sasa ukifananisha na wapinzani wake ambao
wameonekana kutumia fedha nyingi kuimarisha vikosi vyao.
Mpaka
sasa Chelsea wameziba mapengo ya Drogba na Petr Cech ambao nafasi zao
zimejazwa na Asmir Begovic na Radamel Falcao, ambao pia ndio wachezaji
pekee waliosajiliwa na Chelsea.
Wapinzani
wao wametumia mamilioni ya shilingi ikiwepo pauni milioni 49 ambayo Man
City wametoa ili kunasa saini ya Sterling, lakini Mourinho bado
anaamini hahitaji nyongeza katika kikosi chake.
"Ni hatari sana", aliwaambia waandishi wakati alipoulizwa kuhusu ukoefu wa majina mapya ndani ya Stamford Bridge.
"Nadhani
mnachosema ni sahihi, kuna msemo unaosema: 'mchelea mwana utakuta mwana
si wako'. Ni sahihi, lakini watu hao hao wnaweza kuanguka.
"Huhitaji
kununua watu 10 ili kuwa na timu bora. Unaweza kuwa na timu bora kwa
kuongeza mchezaji mmoja au wawili tu, ukichanganya na waliokuwepo basi
mambo safi kabisa".

Comments
Post a Comment