Kuhusu ubora wa Coquelin, Wenger amesema haya.
Arsene Wenger amesisitiza kuwa kwa upande wa takwimu, Francis Coquelin moja ya viungo bora wa ulinzi barani Ulaya.
Coquelin
ametokea kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Arsenal katika miezi ya
hivi karibuni, kufuatia ujio wake kutoka klabu ya Charlton Athletic
mwezi Desemba ambapo alikuwa akikipiga kwa mkopo.
Mfaransa
huyo ameshacheza michezo mitatu mikubwa ya ligi kuu Uingereza mpaka
sasa msimu huu, lakini alikosolewa na machambuzi wa kituo cha
Televisheni cha Sky Sports Gary Neville katika maandalizi ya mchez0
dhidi ya Liverpool, ambapo walitoka suluhu, lakini Wenger amemkingia
kifua na kusema kinda wake huyo ni mchezaji maridadi.
Kwa
uhakika kabisa, Wenger anaamini kwa namna takwimu zinayoonesha, basi
Coquelin ni mchezaji bora ulimwenguni katika nafasi yake.
“Coquelin
ana takwimu nzuri sana kwenye upande wa eneo kiungo wa ulinzi barani
Ulaya. Nadhani huwa mnaangalia mpira kama ambavyo huwa naangalia. Mimi
sijui watu huwa wanaona nini. Kwa upande wa ulinzi, Coquelin anafanya
kazi kubwa sana”, Wenger aliwaambia waaandishi.
“Hebu
angalia, siku zote sipo kinyume na maoni ya mtu. Watu wanaweza kusema
kwamba hawadhani kwamba Arsenal ni timu bora. Nakubaliana nao. Lakini ni
hatari sana kusema kwamba 'Kamwe yule hawezi kuwa mchezaji’ — hasa
maoni hayo yanapotoka kwa watu wanaoufahamu mpira.
“Ndio,
mimi hainiudhi hata kidogo, lakini ninachokisema hapa ni kwamba, hii
inaongeza msukumo kwa wachezaji. Naamini kwamba tupo katika shughuli za
kimpira na tutapambana tu.
"Watu
ambao wamekuwa katika mchezo huu, napenda namna wanavyoenda kwenye
televisheni kuuchambua mpira zaidi. Lakini ningependa wawasaidie watu
kuupenda mpira na sio kuuchukia mpira”.
Hizi ndizo takwimu za Coquelin;
Hizi ndizo takwimu za Coquelin;

Comments
Post a Comment