jose mourinho amkejeli tena wenger
Jose Mourinho amechukua muda wa kumrushia maneno bosi wa Arsenal Arsene Wenger baada ya Mfaransa huyu kukataa mkono wake katika fainali ya Community Shield uwanjani mwa Wembley siku ya Jumapili.
Kocha Mfaransa hatimaye alimpiga Jose Mourinho ambapo Alex Oxlade-Chamberlain alifunga bao katika kipindi cha kwanza na kuipatia Arsenal ushindi wa 1-0 dhidi ya Chelsea katika Community Shield.
Lakini Mourinho amemshitaki mwenzake kutokuwa na heshima baada ya kutokubali mkono wake.
"Mtazamo wangu ni: kitu kimoja ni mitaa na Jambo jingine ni uwanja wa soka," Mourinho alisema.
"Kama mkufunzi katika uwanja wa soka, mimi sikuwahi kukataa kamwe mkono wa mpinzani. Kwa heshima ya klabu yangu na kwa heshima ya soka sitawahi kukataa kamwe mkono wa meneja katika uwanja wa soka. "
Chelsea itaanza kutetea taji lao la Ligi Kuu ya Uingereza siku ya Jumamosi dhidi ya Swansea City.

Comments
Post a Comment