Arsenal kumsajili Gonzalo Higuain
Arsenal yazua mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain na klabu ya Italia yaripotiwa kuwa wanatarajia staa kuitenga klabu.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alikuwa amehusishwa na kuhamia Arsenal kabla hajasajiliwa na Napoli akitokea Real Madrid mwaka 2013.
Mwajentina wa kimataifa, aliyetumia misimu miwili iliyopita katika klabu ya Serie A, alitolewa mkataba mpya na Napoli lakini alikataa na wakala wake Nicolas Higuain alieleza hali hiyo.
"Tulikutana na Rais [Aurelio De Laurentiis] katika Venice siku 10 zilizopita," alisema Nicolas Higuain.
"Kuliongea kuhusu kila kitu. Alitoa mkataba wa mwaka mmoja, hata hivyo, kwa maoni yangu - na kwa maoni yetu - tutaendelea na mkataba wa awali, utakaomalizika mwaka 2018.
"Sidhani kama tutakubali ofa ya rais, kwa sababu mkataba hauna tofauti na ule tuliosaini kabla, hivyo kwetu siyo ofa halisi."
Kwa mujibu wa Metro, Arsenal yazua tena mpango wa kumsajili Higuain, ilhali walijaribu kumsajili Karim Benzema na wakashindwa vita hiyo.
Higuain alifunga mabao 53 katika mechi 102 kwa Napoli tangu ajiunge na klabu kutoka Real Madrid kwa kitita cha €40,000,000.

Comments
Post a Comment