Angel Di Maria afuzu kujiunga na PSG
Angel di Maria ameeleza furaha yake kwa kujiunga na Paris Saint Germain baada ya kufuzu vipimo vya afya yake katika Quatar, ingawa kuhama kwake kutoka Manchester United bado hakujathibitishwa.
Mwajentina wa Kimataifa hatimaye amefuzu vipimo vya afya jijini Doha nchini Qatar siku ya Jumanne na anatarajiwa kujiunga na mabingwa wa Ufaransa katika masaa 24 kwa ada ya £44m.
"Nina furaha sana kujiunga na PSG. Ninachojua kuhusu PSG ni kwamba ni timu ambayo iliyoshinda mataji yote yanayowezekana katika Ufaransa msimu uliopita. Hivi ni muhimu sana kwa klabu. Najua pia kwamba nataka kutinga kikwazo ambacho ni kupita robo fainali ya Ligi ya Mabingwa,'' aliiambia BeIN Sports.
"Nitajaribu kuleta ubora wa uwezo wangu kwa kujiweka katika huduma za timu hii. Tutajaribu na tufike mbali iwezekanavyo katika Ligi ya Mabingwa."
Di Maria alijiunga na Manchester United msimu uliopita akitokea Real Madrid kwa rekodi ya ada ya £59.1m katika Uingereza.

Comments
Post a Comment