Waraka wa Mchungaji Mtikila kwa Edward Lowassa
KATIKA UCHAGUZI MKUU HUU TUSIRUHUSU MAFISADI WALICHEZEE TAIFA
Edward
Lowassa ni balaa kwa Taifa! Democratic Party (DP) inatarajia kufikisha
Mahakamani chama cha CCM pamoja na wanachama wake sita, Edward Lowassa
na wengine, kwa mujibu wa Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania,
kwa kosa kubwa sana la kuvunja Katiba na Sheria za Nchi kwa kuanza
kampeni ya Uchaguzi kabla ya wakati unaopasa kwa mujibu wa Sheria.
1
Tunao ushahidi mzito unaothibitisha kwamba Edward Lowassa na wenzake
walianza kampeni ya urais ndani ya chama chao kabla ya wakati, na kwamba
chama chao kiliwapa adhabu ya kutofanya siasa kwa miezi 12. Lakini
safari hii Lowassa ameanza kampeni ya urais Arusha kwa mkutano mkubwa
sana wa hadhara wa kampeni haramu na kumwaga rushwa ya kutisha!
2
Kama ni wadhamini alipaswa kuwapata katika ofisi za chama chake, katika
mikoa nane (8) tu Tanganyika na mikoa miwili tu Unguja na Pemba,
wadhamini 45 tu katika kila mkoa. Lakini Edward Lowassa amefanya
mikutano nchi nzima, ya kuwaahidi maelfu ya wananchi katika kila mkutano
wa hadhara, mambo atakayofanya kama wakimpa kura zao awe Rais! Hii
ndiyo kampeni halisi, ambayo ni ukiukaji wa Katiba na Sheria za Nchi!
Uchaguzi Mkuu unaendeshwa na Sheria, hivyo ni lazima Sheria ichukue
mkondo wake dhidi yake kwa kuivunja.
3
Edward Lowasa amevunja Katiba ya Nchi na Sheria ya kiwango cha fedha
kinachoruhusiwa kutumika katika shughuli halali za Uchaguzi, kiasi
kwamba CCM na Taasisi zote za uchunguzi wa kifedha nchini, upelelezi wa
Jinai na Usalama wa Taifa ni mlazima wanayo kazi muhimu sana ya kupata
ukweli kuhusu haya mabilioni ya fedha yanayomwagwa nchini na fisadi
Edward Lowasa, ameyapata wapi na kwa namna gani, kumehusika ‘’Money
laundering’ au la, kama mapato ya mapesa hayo yote ni halali, na kama
mapato hayo yote yalilipiwa kodi inayopasa kwa ajili ya Taifa. Ni
marufuku kabisa tena ni makufuru Edward Lowasa kuruhusiwa kugombea
urais, kwa sababu amevunja Katiba ya Nchi na Sheria na Kanuni za
Uchaguzi. Sifa mojawapo ya kustahili kugombea uongozi wa nchi yoyote ni
maadili mema na uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na taratibu za Utawala wa
Sheria
4
Edward Lowasa, kwa kujimilikisha maeneo nchi nzima kwa kutumia kifisadi
Uwaziri wake wa Ardhi, ameliweka Taifa katika hatari kubwa ya mmwagiko
wa damu baina ya wakulima na wafugaji, baada ya kueneza nchi nzima
makundi ya ng’ombe wake, na kusababisha mapigano makali ya mara kwa mara
kila mahali nchini kati ya wafugaji wake na wakulima. Kwa sababu ya
uovu huu hata katika kampeni yake haramu Lowasa ameshindwa kusema lolote
juu ya kilimo, ingawa ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu na
ndiyo shughuli inayotunza uhai wa asilimia 95 ya wananchi! Kwa
kuwaingilia wakulima katika ardhi yao, kuwaua ovyo, kuwaonea kiasi cha
kufisha matumaini yao katika kilimo, kumeifanya kauli mbiu ya “Kilimo
kwanza” kuwa porojo tu ya kisanii!
5
Edward Lowasa ni mwiko kabisa kupewa kugombea urais, kwa sababu siyo tu
aliutumia kifisadi Uwaziri wa Ardhi akajitajirisha na kujipatia maeneo
makubwa ya ardhi nchini kote, bali alitumia kifisadi zaidi uwaziri wa
nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu, katika uagizaji wa mashangingi ya
Wabunge, mawaziri, wakuu wa Mikoa na Wilaya.
6
Edward Lowasa alikemewa mnamo mwaka 1995 na Mwalimu Nyerere anayeenziwa
na CCM lama “Baba” yao, alipotaka kugombea urais, kwa sababu alikuwa
fisadi papa, wala hakuweza kujitetea kwavile utapeli wote
aliojitajirishia ulikuwa mezani. Leo baada ya mabiashara haramu mengi na
kulipora sana Taifa kukiwa ni pamoja na utapeli wa “kununua mvua
Thailand” na kuliibia Taifa mabilioni ya fedha kwa kutumia kampuni hewa
ya RICHMOND, huyu ni fisadi-nyangumi.
Ni
mlemavu wa rushwa tu wa kununuliwa na mapesa machafu anayomwaga Lowasa,
anayeweza kumruhusu fisadi Edward Lowassa agombee urais. Sifa za mtu wa
kukugombea Urais zimeelezwa bayana na Mwenyezi Mungu katika Kumbukumbu
la Torati 17:15-20, ambazo Edward Lowasa hana hata mojawapo! Lowasa
awali alikemewa na Mwalimu Nyerere ambaye CCM wanamuenzi kama “Baba”
yao, kuwa hafai kabisa kuwania urais, kwa sababu alikuwa fisadi papa,
kama alivyomtangaza hata Reginald Mengi pale alipolazimika kujiuzulu
Uwaziri Mkuu kwa ajili ya wizi kwa kampuni hewa ya Richmond, lakini leo
akiwa fisadi la kutisha zaidi kuliko papa eti anataka urais!
Si
ajabu kwamba magabacholi yalioipora vibaya sana Nchi hii kama Sigh
Setti na hata Nazir Karamagi wote wamo katika genge la Edward Lowasa! Si
ajabu hata fisadi Reginald Mengi leo kuungana na fisadi Lowasa
yakizingatiwa machafu yake yeye mwenyewe, na kuhusika kwa Mengi na
mauaji ya Chacha Wangwe, pamoja na mpango wa Chadema wa kumwua Mchungaji
Mtikila, waraka feki wa kujaribu kuupotosha ukweli ukatangazwa kwa ITV
yake.
Katika
uwaziri wake katika ofisi ya Waziri Mkuu, na katika Uwaziri wake wa
Ardhi na Uwaziri Mkuu, Lowasa alifanya ufisadi ambao katika nchi kama
China zenye uchungu na maslahi ya mataifa yao angekuwa wa kupigwa risasi
hadharani, lakini katika nchi yetu anatafuta urais!
7.
Edward Lowasa AFYA yake imempiga marufuku kugombea Urais! Kwa ajili ya
kila ajira duniasni kote, moja ya mashart makuu ni lazima mwombaji awe
na afya iliyo bora, ndiyo sababu ni lazima ajira ya kila mwombaji
itegemee taarifa ya kitaalamu ya madaktari, inayothibitisha kwamba hana
dosari kiafya. Sharti hili ni la lazima kwa sababu:
a.
Majukumu yote atakayopewa mwajiriwa atayatekeleza kikamilifu kwa
kutumia viungo vya mwili wake, kwahiyo viungo vyake vyote ni lazima viwe
katika hali iliyo imara kwa ajili ya kazi.
b.
Hata kama kwa uthibitisho wa kitaalamu wa madaktari mwajiriwa anazo
akili nzuri kichwani mwake, akiwa na hitilafu katika viungo vingine vya
mwili wake huathiri afya ya akili zake na uwezo wa utendaji wa akili
zake.
c.
Kazi ya Rais ni ngumu sana, kwa sababu ni pamoja na kusimamia shughuli
zote za maendeleo ya nchi nzima, na matatizo yote yanayowatokea wananchi
wote kila walipo, na kusimamia utekelezaji wa majukumu yote ya
watendaji wote katika Taifa, hivyo kwamba maamuzi sahihi yanatokana na
afya bora yenye kuhakikisha uwezo unaopasa wa kiakili wakati wote
d.
Hitilafu katika afya hudhoofisha uwezo wa kifikira na kusababisha
maamuzi mabovu, ambayo huleta athari mbaya sana kwa Taifa. Na udhaifu
huo huathiri mpaka maadili na hata uzalendo wa huyo kiongozi mdhaifu.
Kwa mfano akipatikana Rais anayeishi kwa matumaini, kwa hofu ya kupoteza
uhai kabla hajaweka sawa mambo yake na ya familia na jamii yake
atatumikia maslahi yake zaidi kuliko Taifa, tatizo hilo la afya likawa
limelikosesha Taifa kipaumbele, na kuliangamiza kimaendeleo!
e.
Wanaowania kugombea urais ni lazima wachunguzwe kwa makini sana afya
zao, kwa sababu kukifanyika makosa akatawazwa mwenye hitilafu za kiafya,
atakwenda kuwa mzigo mzito sana kwa Taifa, hususan ugharamiaji wa
utunzaji wa uhai wake ndani na nje ya nchi, kukosekana na umakini
anaopasa kuwa nao kwa ajili ya dhamana kubwa aliyopewa n.k. Kutokana na
AFYA yake kuwa dhaifu sana hata kwa kumwona kwa macho tu, kabla ya
uchunguzi wa kitaalamu ni kwamba Edward Lowasa hawezi kabisa kugombea
Urais. Kwani amekosa sifa muhimu sana ya afya bora, ambayo ni ya lazima
kwa mtu yeyote anayestahili kupewa dhamana kubwa sana ya kuliongoza
Taifa. Pengine hata kugombea urais kwenyewe anatafuta kutokana na
hitilafu ya kiafya, iliyosababisha udhaifu katika kufanya maamuzi, hivyo
amejikuta kwa bahati mbaya anagombea asichokiweza kabisa.
Ni
lazima wagombea wote wa Urais, wa Ubunge na hata wa Udiwani wachunguzwe
kwa makini afya zao kabla ya kupewa kugombea, na hata kuchunguzwa tena
katikati ya muhula wa utumishi wao, kama kweli tunalithamini na
kuliheshimu Taifa. Sifa za urais ni wito au uhanga kwa ajili ya Nchi
ambao ni zaidi ya maadili ya kizalendo, maono, vipawa na AFYA BORA.
Ni
dhana potofu sana kwamba sifa ya urais ni kushabikiwa na umati wa watu!
Kwa sababu wengi hufuata mapesa na husombwa hata na magari ili umati wa
kishabiki tu upatikane. Lakini kumpenda mtu huwa lazima kuwe na sababu,
wakati ushabiki ni pepo mchafu au ‘psychological deficiency’. LOWASA NI
MOJAWAPO WA WAGONJWA WA MAGONJWA SUGU WA;IOKUWA WANATIBIWA NA BABU WA
LOLIONDO NA TANGIA PALE HAJAPONA NA ZAIDI SANA ANAANZA KUTETEMEKA

Comments
Post a Comment