Raheem sterling kufanyiwa vipimo leo kabla ya kusaini MANCHESTER CITY
Raheem Sterling kupitia uchunguzi wa kimatibabu leo hii kabla asaini kwa Manchester City
Raheem Sterling atapitia uchunguzi wa kimatibabu leo hii baada ya Liverpool kufikia makubaliano na Manchester City kwa ada ya uhamisho ifikayo £49m kumsajili kijana Mwingereza.
Mingereza wa Kimataifa alihusishwa na kuondoka klabu ya Merseyside kwa kipindi cha miezi michache iliyopita baada ya kutupilia mbali kandarasi mpya ya £100,000 kama mshahara kwa wiki ili akae Anfield.
Kwa mujibu wa Telegraph, Sterling alipata kuwa mchezaji Mwingereza ghali zaidi kwa kusajiliwa na klabu nyingine ya Uingereza baada ya Liverpool na City kukubaliana kitita cha £49m mwishoni mwa wiki.
Ripoti pia yadai kuwa Sterling, ambaye hakusafiri kwa Thailand na kikosi cha Liverpool kutayarisha msimu ujao, anatarajiwa kusaini mkataba na Man City wenye thamani ya £200,000 kila wiki, ambapo atakuwa akipata mashahara zaidi ya £10,400,000 kwa mwaka.
Mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na timu chipukizi ya Liverpool kutoka Queens Park Rangers mwaka 2010 na klabu ya Championship itapata asilimia 20 ya ada yoyote Liverpool itakayomuuza Sterling

Comments
Post a Comment