PRESHA INAPANDA,PRESHA INASHUKA "CCM ",MAMBO YAMEIVA DODOMA,"USIPOKUWA WEWE,ATAKUWA MWINGINE

Wakati vikao vya juu vya CCM vya kuchuja wagombea urais vikianza leo, hofu na wasiwasi umezidi kutanda miongoni mwa wagombea, viongozi na wanachama wa chama hicho kuhusu namna ya kuikabili minyukano baina ya wagombea hao na kibarua cha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Uchunguzi wa gazeti la Mwananchi umebaini kuwa miongoni mwa mambo yanayoleta hofu na kusababisha presha kuongezeka kila kukicha ni woga wa kufanya makosa katika uteuzi wa ndani, hali inayoweza kukigharimu chama hapo baadaye hasa kutokana na kuongezeka nguvu ya upinzani.
Kutokana na hali hiyo kumekuwa na shinikizo kutoka katika makundi mbalimbali chama hicho kuwa makini kumteua mgombea anayekubalika, msafi na mwenye kuchagulika ambaye atatoa ushindani kwa wagombea wa upinzani, hasa Ukawa.
Vilevile, kumekuwapo na wasiwasi wa baadhi ya wagombea kutishia kukihama chama hicho endapo majina yao yatakatwa, jambo ambalo pia linakiweka njia panda.
Comments
Post a Comment