MOURINHO KUTEMA WAWILI
WAKATI Meneja wa Mabingwa wa England Cheksea wakiwa tayari kuwauza Wachezaji wao Wawili, Manchester United inadaiwa kukaribia kumsaini Kipa Namba Moja wa Argentina.
MOURINHO KUWATEMA WAWILI
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amethibitisha Filipe Luis na Mohamed Salah wataruhusiwa kuhama hivi sasa ikiwa itatokea Ofa ya kuridhisha kwao.
Felipe Luis, Mchezaji wa Kimataifa wa Brazil, alijiunga na Chelsea Mwaka Jana kutoka Atletico Madrid kwa Dau la Pauni Milioni 22.7 na huenda akarudi tena Klabu hiyo hiyo alietokea.
Kuhusu Salah, Mchezaji wa Misri ambae Msimu uliopita alikuwa kwa Mkopo huko Fiorentina, Mourinho alisema hana nafasi nae kwenye Kikosi chake cha sasa ingawa Mchezaji huyo amegoma kubakia na Fiorentina.
Mourinho amesema: "Naona hatima ya Salah iko kwingine ama kwa Mkopo au kuuzwa moja kwa moja kwa Dau linalostahili. Kwa sasa tunao Hazard, Willian, Traore, Moses na Cuadrado, Wachezaji Watano katika nafasi hizo hizo. Ni bora usiwe na Wachezaji wengi.

Comments
Post a Comment