Skip to main content

mbeya city fc kuwatema nyota wake kumi


Nyota 10 waliokuwa sehemu ya kikosi cha Mbeya City Fc msimu uliopita, rasmi hawatakuwepo msimu mpya wa 2015/16 unaotarajia kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi ujao.
Kwa mujibu wa Meneja usajiri wa City, Frank Mfundo, wachezaji hao 10  ambao hawatakuwepo City  wanatangulia idadi nyingine ya watakaoachwa  mara baada ya mazungumzo kati yao na klabu kukamilika mwishoni mwa juma hili.
“Kwenye kikosi cha City msimu huu, Paul Nonga,Deus Kaseke,Peter  Mwalyanzi, Peter Mapunda,Fredy Cosmas,Idrisa Rashird,Lambony Luvanda Ashery,David Burhani, Anthony Matogolo na Deo Julius hawatakuwepo, hii ina maana kuwa wameachwa, hii ni kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuisha mikataba  na hakukuwa na mazungumzo yoyote juu ya mikataba mipya huku wengine kati yao wakiwa tayai wamejiunga na timu zingine” alisema Mfundo.
Katika hatua nyingine  Mfundo amedokeza kuwa kuna wachezaji wengine kadhaa ambao bado wako kwenye mazungumzo ya mwisho na klabu  hivyo taarifa  ya mustakabali wao ndani ya kikosi cha City  itatolewa  mwishoni mwa juma hili mara baada ya mazungumzo kukamilika
taarifa kutoka www.mbeyacity.com

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP