Kubenea apata shavu kubwa, aungana na Kafulila, soma hapa kujua
MKURUGENZI
Mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, Saed Kubenea,
leo anatarajiwa kukabidhiwa tuzo ya ushujaa uliotukuka kutokana na
mchango wake kwa taifa.
Taarifa
kutoka jijini Dar es Salaam na ambazo zimethibitishwa Kubenea mwenyewe
zinasema, Tuzo hiyo itatolewa na shirika moja lisilo la kiserikali,
liitwalo, “Dream Success Enterprise (DSE)” la jijini Dar es Salaam.
Mbali
na Kubenea, wengine wanatarajiwa kutunukiwa Tuzo hizo, ni Mbunge wa
Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi), David Kafulila na mtangazaji wa zamani wa
BBC, Vicky Mtetema.
Kubenea
ambaye pia ni mhariri mtendaji wa magazeti ya MwanaHALISI, MSETO na
gazeti la mtandao – MwanaHALISI Online, atakabidhiwa Tuzo ya Uwazi na
Ukweli.
Naye Kafulila atakabidhiwa Tuzo ya Maono Mapevu; huku Vicky akikabidhiwa Tuzo ya Ubunifu.
“Napenda
kuchukua fursa hii kukupongeza kwa kutunukiwa Tuzo hii adhimu. Natoa
shukurani zangu za dhati kwa mchango wako wa hali na mali katika taifa
letu. Umefaanya kazi kubwa isiyopimika,” anaeleza Mtetema katika taarifa
yake kwa Kubenea.
Anasema,
“…umefanya kazi kubwa kwa manufaa ya wengi licha ya wachache kukupinga
kwa ubinafsi wao na wakati mwingine kuhatarisha maisha yako.”
Mtetema
anasema, Tuzo hii inadhihirisha jinsi gani mchango wa mwanahabari huyo
mwenzake unavyowagusa watu wengi na unavyotambuliwa na watu wanaolitakia
mema taifa hili.
“…usichoke kupigania haki kwa ajili ya wengi. Namuomba Mungu akulinde na aendelee kukubariki,” ameeleza Mtetema.
Taarifa
zinasema, Tuzo hiyi iliyoanzishwa mwaka 2014 na kuzinduliwa tarehe 22
Desemba iliwahi kutolewa kwa aliyekuwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.

Comments
Post a Comment