Real Madrid kupepetana na Barcelona mwezi Novemba na Aprili katika El Clasico
Real Madrid kupepetana na Barcelona mwezi Novemba na Aprili katika El Clasico
Real Madrid na Barcelona zitamenyana katika soka yao ya uhasimu mkubwa katika Santiago Bernabeu tarehe 7 au 8 Novemba na watakutana tena tarehe 3 Aprili katika Camp Nou katita mechi ya marudiano.
Ratiba ya msimu wa ligi 2015-16 katika Hispania imetangazwa, na tarehe za Clasico zilipangwa kwenye raundi ya 12 na 31 ya kampeni 2015-16.
Mabingwa wa La Liga watacheza mechi ya kufungua msimu kuteteataji lao wakitembelea Athletic Club tarehe 23 Agosti na mwishowe watamaliza kampeni yao tarehe 15 Mei kwa kuikalibisha Eibar.
Wakati ambapo Real Madrid siku ya kwanza itasafiri kwa klabu iliyopandishwa cheo hivi karibuni Sporting Gijon na kwa mwisho wa msimu wataelekea Galicia kukabiliana na Deportivo La Coruña katika Estadio Riazor.

Comments
Post a Comment