Javier Hernandez aambiwa kuthibitisha thamani yake Manchester United

Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amemtia changamoto Javier Hernandez amwambia kuthibitisha thamani yake katika Old Trafford baada ya kumaliza msimu uliopita kwa mkopo katika Real Madrid.
“Javier anaweza kujithibitisha mwenyewe tena na sasa Falcao na Van Persie waliondoka, nafasi yake ni bora,” Van Gaal alisema.
Mshambulizi wa Mexico ataungana na wachezaji wenzake wa Manchester United Jumamosi katika michuano ya klabu ya kuandaa msimu nchini Marekani.
Chicharito alipata kushiriki katika mechi 154 kwa Manchester United, huku akifunga mabao 59 tangu ajiunge na klabu mwaka 2010.
Lakini alifanya msimu uliopita kwa mkopo katika Real Madrid, ambapo alifunga mabao nane katika mechi 31 katika mashindano yote.

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP