Hizi ndizo sababu zilizomfanya The Rock aache kucheza mieleka, sasahivi ni yeye na movies tu !

Dwayne
Johnson maarufu kama The Rock ni mwigizaji, producer wa movie na
mchezaji wa mieleka kutoka Marekani aliyejitengenezea jina kubwa kwenye
mieleka na baadae tukaanza kumwona kwenye movie za action Hollywood,
Marekani.
The
Rock alichukua time na kufanya interview na gazeti la Esquire la
Marekani na kuongelea mambo mengi ikiwemo sababu zilizomfanya aingie
kwenye movie na kusahau kabisa ishu za mieleka.

Dwayne Johnson kwenye movie ya The Expendables 3.. Pembeni yake yuko Bruce Wills.
“Baada
ya kufanikiwa kwenye mieleka, nilihamasika kujaribu kucheza movie za
action, na nimefika hapa nilipo kutokana na nidhamu niliyojifunza kwenye
mieleka, kujenga ukaribu na watu kwenye industry, na kujiunga na
madarasa ya kuigiza“>>> Hapa amenukuliwaThe Rock kwenye moja ya
mahojiano yake.

The Rock kwenye action
Anapendelea
nini kati ya mieleka na action movies? >>> “Mieleka ni mpenzi
wangu wa kwanza, lakini kwenye kuigiza kuna upendo tofauti ambao
unaniruhusu mimi kugusa watu kupitia sanaa nyingine na pia kutengeneza
hela ndefu zaidi, movie zinanifundisha mambo mengi sana ambayo
nisingeweza kuyajua mwanzoni“.

Hapa ni kwenye movie aliyoigiza 2015 SAN ANDREAS, moja ya movies ziliofanya vizuri Marekani.
Kuna
mtu alimchukulia serious alivyoanza kuigiza? : “Haikuwa rahisi hapo
mwanzoni… niliambiwa nina mwili mkubwa kuwa mwigizaji wa movie za action
na nilinyimwa nafasi nyingi lakini sikukata tamaa, na leo niko hapa kwa
sababu sikuchoka“.
Comments
Post a Comment