Habari njema kwa Chelsea kuhusu Falcao

Hatimaye Radamel Falcao amesaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Chelsea na ataungana moja kwa moja kujumuika na wenzake katika kipindi hiki cha maandalizi kabla ya msimu mpya kuanza huku nchini Marekani (Pre-season)
Baba na Mjomba wa Falcao wamethibitisha rasmi habari hizo kwa gazeti la The Guardian kwamba, ni kweli Chelsea wamemsajili mshambuliaji huyo raia wa Colombia.
Kwa mujibu wa gazeti hilo ni kwamba, Falcao atakipiga kwa mkopo kwa mwaka mmoja kama ilivyokuwa kwa Man United huku kukiwa na kipengele cha kumsajili moja kwa moja endapo kiwango chake kitamridhisha kocha wake.
Lakini kwa upande wao Chelsea, bado hawajatangaza rasmi  kuhusu tukio hili la usajili wa Falcao huku tetesi zikisema kuwa, makubaliano ya awali yalikuwa ni FALCAO kupewa kitita cha mshahara wa Pauni 265,000 kwa wiki.
Lakini Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Chelsea zinadai kuwa, watakuwa wakimlipa mshahara wa takriban pauni 180,000 kwa wiki huku ada ya uhamisho wa mkopo ikidaiwa kuwa ni kiasi cha pauni milioni 4
Ikumbukwe tu wakala wa Falcao Jorge Mendes pia ni wakala wa kocha wa Chelsea Jose Mourinho, na Mourinho ameahidi kukirudisha upya kiwango cha Falcao ambacho kimepotea ghafla hasa baada ya kukumbwa na majeraha ya muda mrefu kabla kujiunga na Mashetani Weundu Manchester United msimu uliopita.

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP