Giroud: "Nitaongea na Henry ana kwa ana kuhusu upinzani"

Giroud: "Nitaongea na Henry ana kwa ana kuhusu upinzani"
Mshambuliaji Arsenal Olivier Giroud ametangaza kuwa atamwendea Mfaransa mwenzake Thierry Henry, na kuongea ana kwa ana baada ya maneno ya upinzani kumlaumu kutokuwa na uwezo msimu upitao.
Mhakiki wa Sky Sports Henry alisema mwezi Aprili kwamba Arsenal haiwezi kushinda ligi pindi wangali na Giroud kama straika. Na alitangaza hivyo wakati Arsenal ilitoka sare ya utasa wa mabao dhidi ya Chelsea mwezi Aprili.
"Kwa uaminifu, unapokuwa mwanasoka hupaswi kusikiliza watu wanaotoa maoni kuhusu utendaji wako," Giroud aliwaambia watangazaji habari.
"Jambo muhimu ni kutokuwa na shaka yoyote unapokosea bahati au kutocheza mechi. Inaweza kutokea wakati mwingine.
"Jambo bora ni kusahau maoni mara kwa mara na usidhoofike na usiyaruhusu aathiri sifa zako. Mimi namjua Thierry na nilijua kile alichotaka kumaanisha. Nitakapomwona tutakuwa na mazungumzo kati ya wanaume wawili. .
"Sina hasira dhidi yake lakini ni kweli kwamba sikuelewa kwa mara ya kwanza. Nadhani alifikiria tena kuhusu maneno yake na kuyaeleza zaidi. Lakini inatosha. Hilo halitaniletea vurugu. Ninalala vizuri na kama familia yangu ni sawa hilo ni jambo muhimu. Haitaniathiri kupita kiasi."
Giroud alifunga mabao 58 katika mechi 134 kwa Arsenal tangu ajiunge na klabu kutoka Montpellier mnamo 2013.

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP