ferguson : juventus muuzeni pogba
Sir Alex Ferguson aiambia Juventus kumuuza Paul Pogba
Aliyekuwa kocha kabambe wa Manchester United Sir Alex Ferguson anaishauri Juventus kumuuza Paul Pogba katika kiangazi hiki kabla Mfaransa aondoke klabu kwa uhamisho bure.
Mwenye umri wa miaka 22 aliweza kuvutia vilabu kadhaa kutoka Ulaya katika kiangazi hiki, ikiwemo Manchester United, Chelsea na Barcelona.
Lakini Mabingwa wa Italia walisema kuwa mchezaji hauzwi licha ya zabuni ya €80,000,000 kutoka klabu ya Catalan.
"Ndiyo, ningependa kuuza Pogba '' Mskoti amenukuliwa na Tuttosport akisema.
"Ndiyo, ni ukweli mimi tayari nilimpoteza kwa bure, lakini sasa, kama ningekuwa Juve, Ningemuuza."
Wote wawili Ferguson na Pogba walidumu miaka mitatu pamoja katika Old Trafford tangu 2009-2012 kabla kiungo ajiunge na Juve wakati mkataba wake ulikuwa umemalizika

Comments
Post a Comment