Demba Ba ajiunga na Shanghai Shenhua

Demba Ba
Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal Demba Ba amejiunga na timu ya Shanghai Shenhua akitokea timu ya Besiktas ya Uturuki.
Ba
mwenye umri wa miaka 30 alikua anatarajiwa kurudi katika ligi kuu ya
England, lakini ameamua kuelekea mashariki ya mbali kusakata kabumbu.
Mchezaji
huyu wa zamani wa vilabu vya Newcastle na Chelsea, alifunga mabao 27
katika michezo 44 aliyoicheza timu ya Besiktas, msimu uliopita.
Nyota
huyu wa kikosi cha simba wa Teranga (Senegal), nyota yake ilianza
kungara mwaka 2005 katika klabu ya Rouen kabla ya kuelekea Ubelgiji
alikocheza kwa msimu mmoja katika timu ya Mouscron.
Baadaye
akatimkia Ujerumani kwa miaka 4 akiitumika klabu ya Hoffenheim msimu wa
2011 akajiunga na wagonga nyundo wa London West Ham.
Baada
ya kufanya vizuri na West Ham akajiunga na Newcastle katika msimu wa
2011/12alipofunga mabao 29 katika michezo 57 kabla ya kuhamia Chelsea na
kucheza michezo 51 akizifumania nyavu mara 14.
Comments
Post a Comment