AZAM YAANZA KUMPIGIA HESABU ‘MESSI


Messi-Singano1.jpgAzam FC ni klabu ambayo imekuwa ikihusishwa kutaka kumsajili mchezaji Ramadhani Singano ‘Messi’ hasa baada ya mkataba wa mchezaji huyo na Simba kuvunjwa jana na kamati ya sheria na hadhi za wachezaji baada ya kukudulika kuwa Simba ilishindwa kutimizia majukumu yake ambayo yalikuwa yameainishwa kwenye mkataba wao.
Mtendaji mkuu wa Azam FC Saad Kawemba amesema, wao wanamsikiliza mwalimu wao Stewart Hall kama atakuwa anamuhitaji mchezaji huyo basi wako tayari kukaa na kufanya mazungumzo na mchezaji ili awasaidie kwenye msimu ujao.
“Tunachokisema toka mwanzo ni kwamba, kijana ni mchezaji mzuri na kila klabu ingependa kuwa naye, lakini jambo jema tunashukuru Mungu kesi yake imekwisha na yuko huru. Sasa ni jukumu la kijana mwenyewe kuweza kuamua ila kama ikituhitaji sisi hatuna tabu akisema anamapenzi ya kucheza kwetu  na walimu wakimkubali itakuwa ni heri”, amesema Kawemba.
“Lakini hatuna sababu ya kusema kwamba kwa vile yuko huru basi ‘automatically’ anakuja Azam. Azam ni timu inayoheshimu mikataba ya vilabu vingine, mchezaji alikuwa bado anamkataba na Simba na mwenye mamlaka ya kusema mkata ni halali au sio halali ni kamati ya sheria na hadhi za wachezaji na imefanya hivyo kwasababu ndio wenye mamlaka hayo ya kisheria kimpira”, alifafanua.
“Kwahiyo, wakati kesi inaendelea tulikuwa hatuwezi kufanya mazungumzo kwasababu kufanya hivyo ilikuwa ni kuvunja kanuni za usajili. Mwalimu akisema kwamba anamuhitaji, tutafanya nae mazungumzo na kama mchezaji pia atakuwa na ‘interest’ ya kuwa na sisi kwasababu hicho ni kitu muhimu sana sio kumchukua mchezaji ambaye hana mapenzi na nyie”, ailongeza.
“Tunamsikiliza mwalimu wetu, kwasababu mwanzo tulisema tutasajili mchezaji mmoja wa ndani na tumeshamsajili Ame Ally kwahiyo ‘target’ zetu zote ziko nje na tunaendelea nazo sasa kwa ndani ikitokea hiyo mwalimu akisema naye ni miongoni mwa watu anaowahitaji tutafanya mazungumzo na wasimamizi wake kuona kama ataweza kutusaidia”, alimaliza.
Mbali na Azam, inasemekana klabu ya Yanga nayo inamnyatia mchezaji huyo ili kuinasa saini yake.

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP